ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 18, 2012

SAKATA LA UCHOMAJI NYUMBA 55 HIFADHI YA TAIFA WILAYANI MAGU MKUU WA WILAYA HIYO AZUNGUMZA

Msikilize Mkuu wa wilaya ya Magu Bi. Jaqueline Liana kwa kubofya play:- 

Friday, August 17, 2012

FAMILIA 55 ZACHOMEWA NYUMBA WILAYANI MAGUHali halisi.


KAYA  55 Wilayani Magu, mkoa wa Mwanza hazina mahali pa kuishi baada ya nyumba zao zaidi ya 90 kubomolewa kisha kuchomwa ikiwa ni sehemu ya kutimiza amri ya serikali nyumba hizo kubomolewa kupisha eneo hilo linalotajwa kuwa ni hifadhi ya taifa.
Tukio hilo la kinyama linadaiwa kufanyika kuanzia tarehe 1 Agosti hadi Agosti 2 mwaka huu, ambapo zioezi hilo liliendeshwa chini ya usimamizi wa mkuu mpya wa wilaya hiyo Jaquline Liana akishirikiana na jeshi la  polisi wilayani humo.
Wakizungumza na g sengo blog kuhusiana na tukio hilo, wananchi hao wameilaumu serikali kwa kusema kuwa imeonesha ukatili wa hali ya juu kwa kuwavunjia nyumba zao,  ile hali wakijua kabisa hawana uwezo hata wa kujenga mabanda kwa mifugo iwe vipi ndani ya muda wa wiki mbili wawe na mtaji kujenga nyumba za kuishi?.. hakika ni kitendo ambacho kinakiuka haki za binadamu na utawala bora.
Wamesema kuwa askari hao walitumia silaha za jadi kuvunja na kuchoma moto nyumba zao.


Moja kati ya waliovunjiwa na kuchomewa nyumba zao Bw. Paulo nkiligila akiwa na familia yake asijue wapi pa kujisitiri, zaidi ya kuishi chini ya minyaa
Ilielezwa kuwa kuvunjwa kwa nyumba hizo za vijiji vya Mwabulenga, Misungwi,Bugalu  na Salama ni sehemu ya mikakati ya serikali kutaka kugeuza eneo hilo la Sayaka kuwa  hifadhi ya taifa, ambayo wananchi hao wanadai wamekuwapo zaidi ya  miaka 70 tangu enzi za babu zao.


Eneo hili la mbele lilichochomwa lilikuwepo zizi la ng'ombe kwa sasa vimebaki viashiria tu.. vya historia.


Pichani ni Emmanuel James Salala ambaye ni Mjumbe wa Serikali ya kijiji Msikilize kwa kubofya Hapa
Mmoja wa wathirika wa tukio hilo, Manhe Mayoka (80) alisema ameishi hapo akirejea nja ya mwaka 1940 anashangaa leo eneo hilo wanaambiwa wapishe ni hifadhi ya taifa, mzee huyo amevunjiwa nyumba zake tatu.


Moja kati ya familia zilizo athiriwa na bomoa na nyumba zao kuchomwa moto kutoka kushoto Kija Mahenhe, Rebeca Mahenhe, Maria Mahenhe, Mariam Manhungwa na mtoto aliyebebwa ni Clement. Familia hii imejisitiri pembezoni mwa kuta za mwenyekiti wa kitongoji cha Itongo kijiji cha Bugatu wilayani Magu Bw. Kulwa Ezekiel  


Wananchi walioathiriwa na kadhia hiyo ni wa vijiji vya Misungwi Kata ya Sukuma na katika kata ya   Ng’aya ni , Mwabulenga, Salama  na Bugatu  wilayani Magu na baadhi ya vijiji vya wilaya ya busega.


Hii ndiyo himaya wa mwenyekiti wa kitongoji cha Itongo kijiji cha Bugatu wilayani Magu Bw. Kulwa Ezekiel 


Haya ndiyo maisha ya wananchi hawa waliovunjiwa nyumba zao kisha kuchomewa, wamekusanya baadhi ya makuti ya nyumba yao ya zamani na  matofali kisha wakatengeneza kingo na hapo ndipo wanapolala. 


Huyu na familia yake ameamua kuhama la faa lake la kuhifadhia chakula akijihifadhi pembezoni mwa nyumba ya mwenyekiti kusubiri ujenzi wa nyumba yake mpya ambao hata hivyo hajajuwa wapi pa kujenga na atajengaje ile hali hakupata hata fidia kama mtaji wa ujenzi.


Pa kujisitiri familia 


Licha ya kutokujua hatma ya pa kulala vijana hawa kamera yako iliwanasa wakijisomea kulia ni Ndutu Samson (20) anayesoma kidato cha 4 na Bukong'one Zacharia (16) anayesoma kidato cha 3, wote katika Shule ya sekondari Ng'aya wilayani Magu. 


Hapa palikuwa bafu.. si waona jiwe la kujisugulia?


Hali tete....


Wamevunja nyumba zooooote za kizungu lakini hiki kijumba wamekibakiza ... "Au ni Yale mambo ya Vunja Uone?"
by G. Sengo


Ni familia ya watoto watano ya Bi. Sabina Joseph katika makazi mapya.


Naye huyu akiwa na mwanaye na mumewe hayuko pichani ambao wanatajwa kuwa walifunga harusi hivi karibuni tu na kupata mtoto huyo kilichofuata nyumba ikabomolewa na kuchomwa na sasa wanajisitiri pembezoni mwa kuta za mwenyekiti wao wakisubiri siku isiyofahamika kuishi maisha kama ya awali yaani ndani ya nyumba. 


Mama akihangaika na pichi jiko la nje.Msikilize dada Batinde Nyaruge mmoja kati ya waliovunjiwa nyumba

VYOMBO VYA HABARI VYASHIRIKI SEMINA ELEKEZI KUHUSIANA NA MCHAKATO WA MABADILIKO YA KATIBA MPYA JIJINI DAY LEO.

Mwandishi Mkongwe hapa nchini,Mzee Phill Karashani ambaye aliwahi kupata tuzo ya Maisha ya Mafanikio katika Tasnia ya Habari mwaka 2011,katika tuzo ya Wanahabari Bora wa Mwaka 2011,akifafanua jambo kwenye semina elekezi ya jinsi ya ushiriki wa vyombo vya habari kuhusiana na mchakato wa mabadiliko ya Katiba Mpya iliyowahusu Wanahabari/Wachora Katuni na wadau wengine mbalimbali iliyofanyika kwenye moja ya ukumbi wa Land Mark hotel,Ubungo jijini Dar Es Salaam.Semina hiyo imeandaliwa na Kikundi Cha Sheria na Haki za Binadamu Cha TIFPA kwa Msaada wa Shirika la Ford Foundation la Marekani .
Baadhi ya Wanahabari,Wachora Katuni na Wadau wengine mbalimbali wakifuatilia mada mbali mbali zilizokuwa zikitolewa kwenye semina  elekezi ya jinsi ya ushiriki wa vyombo vya habari kuhusiana na mchakato wa mabadiliko ya Katiba Mpya iliyofanyika kwenye moja ya ukumbi wa Land Mark hotel,Ubungo jijini Dar Es Salaam.Semina hiyo imeandaliwa na Kikundi Cha Sheria na Haki za Binadamu Cha TIFPA kwa Msaada wa Shirika la Ford Foundation la Marekani .hiyo kuhusiana na mchakato wa kutoa maoni kuhusu Katiba Mpya na pia namna ya kuielimisha jamii katika umuhimu wa kushiriki 
Mchora Katuni mahiri Masoud Kipanya na Mmoja wa watangazaji wa kutoka Times FM Radio Ibrahim Issa wakifuatilia mijadala mbalimbali iliyokuwa ikiendelea kwenye  semina elekezi ya jinsi ya ushiriki wa vyombo vya habari kuhusiana na mchakato wa mabadiliko ya Katiba Mpya iliyofanyika kwenye moja ya ukumbi wa Land Mark hotel,Ubungo jijini Dar Es Salaam.Semina hiyo imeandaliwa na Kikundi Cha Sheria na Haki za Binadamu Cha TIFPA kwa Msaada wa Shirika la Ford Foundation la Marekani . 
Naibu Mhariri Mtendaji wa Free Media ambao ni wachapishaji wa gazeti la Tanzania Daima na Sayari, Ansbert Ngurumo akifafanua jambo mapema leo kwenye semina elekezi ya jinsi ya ushiriki wa vyombo vya habari kuhusiana na mchakato wa mabadiliko ya Katiba Mpya iliyofanyika kwenye moja ya ukumbi wa Land Mark hotel,Ubungo jijini Dar Es Salaam,kushoto kwake ni Mwandishi Mkongwe hapa nchini,Mzee Phill Karashani
 Mwenyekiti wa Kikundi Cha Sheria na Haki za Binadamu Cha TIFPA (Chama Cha Wanafunzi waliofadhiliwa na Shirika la Ford Foundation la Marekani) akielezea jambo kwa Wanahabari,Wachora Katuni na wadau wengine mbalimbali kwenye semina elekezi ya jinsi ya ushiriki wa vyombo vya habari kuhusiana na mchakato wa mabadiliko ya Katiba Mpya.
Mijadala ikiendelea kwenye semina hiyo elekezi ya jinsi ya ushiriki wa vyombo vya habari kuhusiana na mchakato wa mabadiliko ya Katiba Mpya
Mwandishi Mwandamizi kutoka Magazeti ya Serikali,Beda Msimbe akifuatilia mijadala mbalimbali iliyokuwa ikitolewa kwenye semina elekezi ya jinsi ya ushiriki wa vyombo vya habari kuhusiana na mchakato wa mabadiliko ya Katiba Mpya.
Washiriki wa Semina hiyo wakifuatilia mijadala iliyokuwa ikiendelea kwenye semina hiyo.
Washiriki wa Semina hiyo wakifuatilia mijadala iliyokuwa ikiendelea kwenye semina hiyo elekezi ya jinsi ya ushiriki wa vyombo vya habari kuhusiana na mchakato wa mabadiliko ya Katiba Mpya.

MWANZA PRESS CLUB YAKAMILISHA SAFU YA VIONGOZI WAKEMATOKEO

Rais wa Chama cha waandishi wa habari Tanzania UTPC Keneth Simbaya akihutubia Mkutano wa uchaguzi mdogo MPC
 Chama cha waandishi wa habari jijini Mwanza hatimaye kime kamilisha safu ya viongozi wake mara baada ya kufanyika uchaguzi mdogo uliofanyika jumatano august 2012 katika ukumbi wa Halmashauri ya jiji la Mwanza kujaza nafasi za uongozi wa chama zilizokuwawazi.


 Nafasi zilizohusika na uchaguzi ni ya makamu mwenyekiti na mhasibu ambapo kwa nafasi ya Uhasibu ilishauriwa wagombea wawe wanawake pekee kwa kuwa katiba ilikuwa ikihitaji mwanamke kutokana na kwamba tayari nafasi tatu za juu zilikuwa na wanaume.


 Fredrick Katulanda aliyekuwa katika nafasi ya Uhasibu aliamua kujiengua ili kuleta changamoto za utendaji naye Flora Magabe aliamua kujiengua kukitumikia cha waandishi wa habari Mwanza katika nafasi ya Umakamu Mwenyekiti kutokana na kuelekeza mahaba yake zaidi kwa Chama cha Mapinduzi ambako kuna nafasi nyeti anagombea ndani ya CCM, na moja kati ya vipengele vya katiba ya MPC vinamtaka kiongozi kutokuwa na nafsi yoyote ndani ya vyama vya siasa.


Mwanahabari Emmy Lema akijinadi kwa wajumbe na wanachama wa MPC ili wampatie dhamana katika nafasi ya Uweka hazina licha ya kuwa na sifa za kutosha lakini kura hazikutosha. 


 Kura zikihesabiwa.


 Hatimaye Denis Mpagaze (kulia) ndiye alitawazwa kuwa Mwenyekiti msaidizi wa MPC kwa kura 38 akimwacha mpinzani wake Emmy Mshana aliyepata kura 9, kura zilizopigwa ni kura 47, kura 1 iliharibika. Pichani Mpagaze akiwa na Makamu mwenyekiti aliye jiuzuru Flora Magabe.


 Makamu mwenyekiti aliyejiuzuru kutokana na kuwa na mahaba na Siasa, Bi. Flora Magabe akipeana mkono na Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mwanza (MPC) aliyechaguliwa katika uchaguzi uliopita Deus Bugahirwa mara baada ya uchaguzi kukamilika. 


Safu kamili.
Nayo nafasi ya Uhasibu imenyakuliwa na mama Adventina Kashalaba (wa  pili mbele kutoka kulia) aliyemshinda Emmy Lema ambaye pia aligombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti. 

TBL YADHAMINI MASHINDANO YA KOMBE LA POLISI JAMII WILAYA YA ILEMELA NA NYAMAGANA MKOANI MWANZA


TBL YADHAMINI MASHINDANO YA KOMBE LA POLISI JAMII WILAYA YA ILEMELA NA NYAMAGANA MKOANI MWANZA.
Regional Crime Officer-Mwanza Joseph M. Konyo akipokea kitita cha shilingi milioni moja kutoka kwa meneja matukio wa kanda ya ziwa Erick Mwayela, ili kufanikisha mashindano ya kombe la polisi jamii wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.

Afisa upelelezi Patrick Kimaro akipokea pesa taslim sh 1,000,000/= kwa niaba ya Mkuu wa Polisi wilaya ya Ilemela kutoka kwa meneja matukio wa kanda ya ziwa  Erick Mwayela kwa ajili ya mashindano ya Polisi jamii ya wilaya ya Ilemela Mwanza. 

BONDIA SANDE KIZITO TOKA UGANDA AWASILI KUMKABILI RAMADHANI SHAURI SIKU YA IDI PILIBondia Sande Kizito wa Uganda
Bondia Sande Kizito katikati akiwa amewasili katika jiji la Dar es salaam usiku wa leo akitokea Uganda kwa ajili ya mpambano wakena Ramadhani Shauri siku ya Idi pili kushoto ni mwenyeji wake aliyempokea Yasini Abdallah 
Bondia Sande Kizito akiwasili akitokea Uganda kwa ajili ya kumkabiri mpinzani wake Ramadhani Shauri la kugombea ubingwa waIBF Africa litakalofanyika siku ya Idi pili 
Bondia Sande Kizito wa Uganda kulia akiwa na kocha wake Bogere Francis baada ya kuwasili usiku wa leopicha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Thursday, August 16, 2012

UFUNGUZI WA MATAWI YA CHADEMA MAREKANI


UFUNGUZI WA TAWI LA CHADEMA JIJINI HUSTON TX.
Tunapenda kutoa habari hizi kwa waTanzania wote na wapenda maendeleo, Siku ya Jumamosi Aug 25 kutakuwa na ufunguzi rasmi wa tawi la chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Jijini Houston Texas Nchini Marekani, Wageni rasmi wa ufunguzi wa tawi hilo ni Mhe. Freeman Mbowe na Mhe. Jodeph Mbilinyi (Mr. 2/Sugu) Sherehe za ufunguzi wa tawi hilo zitaanza mida ya saa 5:PM (Jioni)

SKYLIGHT BAND KUTAWAMBULISHA WAKALI WAO SIKU YA EID MOSI NA PILI NDANI YA GIRAFFE OCEAN VIEW, DAR

 Vijana wa kazi walionyesha staili yao mpya ya kuheza.
NA MWANDISHI WETU 
WASANII wa muziki wa kizazi kipya Mwasiti Almasi na Zena Mohamed ‘Shilole’ wanatarajiwa kusindikiza uzinduzi wa bendi ya Skylight wakati wa Sikukuu ya Iddi Mosi. 
 Akizungumza na vyombo vya habari jana kiongozi wa Skylight Band Aneth Kusila ‘AK47’ alisema uzinduzi huo utafanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Giraffe, uliyopo Mbezi Beach. 

AK47 alisema uzinduzi huo utakuwa wa namna yake kutokana na uwezo mkubwa walionao wasanii wanaounda Skylight. “Mashabiki wote wa muziki Tanzania waje washuhudie vipaji hivyo na jinsi tulivyojiandaa kuwapa burudani ya aina yake,” alisema AK47. 

Skylight Band inaundwa na wakali kama AK47 na Mary Lucos, ambaye aliwahi kushiriki mashindano ya Bongo Star Search (BSS). 

Wengine ni Joniko Flower na Sam Machozi, ambao wote wametoka Machozi Band, inayomilikiwa na Lady Jay Dee. 

Baada ya uzinduzi huo Skylight Band watafanya onyesho jingine kwenye ukumbi huo wa Giraffe siku ya Iddi Pili, ambapo Dj Nelly ataonyesha uwezo kwa kupagawisha mashabiki kwenye maonyesho yote mawili.