Ligi kuu ya England inazidi kupamba moto, huku Arsenal wakiendelea kukalia kiti cha uongozi, baada ya kupata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Cardiff City.
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, anasema:
"Tunajua tutacheza michezo 10 hapa nyumbani na tunataka kuifanya sehemu hii kuwa ngome yetu, bila kujali wengine wanafanya nini.
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, anasema:
"Tunajua tutacheza michezo 10 hapa nyumbani na tunataka kuifanya sehemu hii kuwa ngome yetu, bila kujali wengine wanafanya nini.
"Iwapo tunaweza kufanya hivyo, tutakuwa katika nafasi nzuri zaidi."
Arsenal, haiko salama sana katika nafasi yake ya kwanza ikiwa na pointi 45, kwani kwa karibu sana inanyemelewa na Manchester City yenye pointi 44, huku Chelsea ikiweka kibindoni pointi 43 ikiwa katika nafasi ya tatu. Liverpool imejisogeza juu kutoka nafasi ya tano sasa iko nafasi ya nne baada ya kujikusanyia pointi 39, huku Everton ikipigwa kumbo na kusogezwa nafasi ya tano kwa kuwa na pointi 38. Wakati Tottenham ikipanda juu katika nafasi ya sita kwa kupata pointi 37, mabingwa watetezi Manchester United imesukumwa chini hadi nafasi ya saba kwa kukusanya pointi 34.
Wakati timu hizo zikipigana kufa kupona kunyakua ubingwa wa ligi kuu au kuwemo katika nne bora, timu nyingine zinapigana kuepuka kushuka daraja. Timu zilizo katika hatari zaidi mpaka sasa baada ya timu zote kucheza mechi 20, ni Sunderland iliyoko nafasi ya 20 kati ya timu 20 za ligi hiyo,ikiwa na pointi 14 tu. West Ham inashikilia nafasi ya 19 ikiwa na pointi 15 na Crystal Palace ni ya 18 ikipata pointi 17 na kuipisha Cardiff City katika nafasi ya 17 iliyokuwa inashikilia kabla ya mchezo wa Jumatano.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.