Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) Thobias Andengenye, akipokea Sare za kuzimia moto (Fire suite), kutoka kwa Mwakilishi wa Kampuni ya Wilna International Japan, Bw. Martin Chuwa. Vifaa hivyo vimepokelewa Makao mapema hii leo Makuu Ndogo ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) Thobias Andengenye, akipokea Mikanda maalum kwa ajili ya maokozi (Rescue Belt), kutoka Mwakilishi wa Kampuni ya Wilna International Japan, Bw. Martin Chuwa. Vifaa hivyo vimepokelewa mapema hii leo Makao Makuu Ndogo ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya vifaa vya kuzimia moto na maokozi vilivyotolewa na Kampuni ya Wilna International Japan na kukabidhiwa kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa Lengo la kuboresha utendaji kazi. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Kamishna Jenerali wa
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, CGF Thobias Andengenye, amepokea msaada wa
vifaa vya kuzimia moto na maokozi vitakavyotumika kwa shughuli mbalimbali za
Jeshi hilo.
Amepokea msaada huo
mapema hii leo Makao Makuu Ndogo ya
Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam, kutoka kwa Kampuni ya Wilna International
Japan.
Hata hivyo, Andengenye
ameishukuru Kampuni hiyo kwa kutoa msaada huo na kushirikiana na Jeshi hilo
katika Kuokoa Maisha na Mali za Watanzania.
Aidha, Mwakilishi wa Kampuni
ya Wilna International Japan, Bw. Martin Chuwa, amesema kuwa wameamua kutoa
msaada huo wa vifaa vya kuzimia moto na maokozi ili kurahisisha utendaji kazi
wa Jeshi hilo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.