ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 5, 2019

TBL YASHIRIKIANA NA MUHAS KUFANIKISHA ELIMU YA LISHE KWA WAJAWAZITO NA UGONJWA WA SELI MUNDU (SICKLE CELL)

Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL, Irene Mutingazi akiongea wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo. Rais wa Chama cha Madaktari Tanzaia,Dkt Elisha Osat, (kulia) akichangia mada wakati wa mafunzo hayo, (Kushoto) anayesikiliza ni Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL, Irene Mutingazi. Wadau wanaoshiriki mafunzo wakifuatilia mada mbalimbali kutoka kwa wakufunzi Baadhi ya washiriki wa mafunzo katika picha ya pamoja. Katika mwendelezo wa kuunga mkono jitihada za Serikali kukabiliana na changamoto mbalimbali katika jamii, kampuni ya Bia Tanzania (TBL) imeshirikiana na Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, (MUHAS), kufanikisha mafunzo ya siku 3 kwa wauguzi kutoka hospitali za Dar es Salaam kuhusiana na Afya ya Lishe kwa akina mama wajawazito na ugonjwa wa Seli mundu (Sickle Cell ).

 Akiongea wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo yanayoendelea katika Chuo Kikuu cha MUHAS, Meneja wa masuala Endelevu wa TBL ,Irene Mutingazi,alisema kuwa TBL imejitosa katika kusaidia katika sekta ya afya kama ambavyo imekuwa ikisaidia kukabiliana na huduma changamoto mbalimbali za kijamii kupitia sera yake ya kusaidia huduma za kijamii inayolenga kuwaleta Watu Pamoja Katika Ulimwengu Maridhawa. “Mafunzo haya kwa wauguzi kutoka hospitali za Dar es Salaam tuna imani yatasaidia kupunguza changamoto ya elimu ya lishe duni na ugonjwa wa Selimundo kwa kuwa wataifikisha kwa walengwa wanaowahudumia hususani akina mama wajawazito na wagonjwa wa Seli mundu”,alisema. 

 Aliongeza kuwa TBL kupitis sera yake ya kuifanya Dunia Maridhawa itasaidia kushirikiana na wadau mbalimbali kukabiliana na changamoto mbalimbali katika jamii hususani katika sekta ya elimu na afya. 

 Kwa upande wake, Rais wa Chama cha Madaktari Tanzaia,Dkt Elisha Osat,alisema sekta ya afya inakabiliwa na changamoto mbalimbali na aliwashukuru wadau kama TBL ambao wamekuwa wakijitoa kusaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo katika sekta hiyo. --

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.