ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, August 31, 2017

KUELEKEA SIKUKUU YA EID EL HADJI JESHI LA POLISI DAR ES SALAAM LIMEKUJA NA TAARIFA HII.

Kesho ni siku kuu ya Eid el Hadji, Kamanda wa Polisi wa Kanda maalumu ya Dar es salam SACP Lazaro Mambosasa amepiga marufuku shughuli aina ya Disco toto katika Jiji la Dar es salaam.

Akizungumza leo Jijini humo na vyombo vya habari ameeleza kuwa hatua hiyo imefuta kwakuwa mpaka sasa hawajapokea maombi kutoka kwa wamiliki wa kumbi za starehe kwaajili ya Watoto kwahiyo jeshi la polisi haliwezi kuruhusu bila kujiridhisha kama kumbi hizo zina hewa ya kutosha.
"Nitoe rai kwa wananchi katika sikukuu hii ambayo huitwa sikukuu ya kuchinja, tunawaomba wananchi washerehekee pamoja na familia zao lakini uangaliazi kwa watoto uwe ni wa hali ya juu, wasiwaache watoto wadogo kuingia kwenye kumbi za starehe au kwenda maeneo mengine ambayo kimsingi ni hatarishi kwa watoto hao" BOFYA PLAY KUMSIKIA

Hata hivyo Mambosasa amewahakikishia Wakaazi wote wa Jiji la Dar es es salaam kuwa wamejipanga vyema kuhakikisha sikukuu hiyo inamalizika kwa amani utulivu

Sambamba hilo amewataka Wana Dar es salaam kushirikiana na jeshi hilo ili kufichua vitendo vya kihalifu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.