Mkurugenzi Mkuu wa TDL akiwa na Mabosi wa SABMILLER AFRICA.wakiwa wameshikilia tuzo hiyo ya MB COMPLEMENTARY BEVERAGE CATEGORY AWARD FOR (F 13)
|
PICHA NDOGO CHINI NI BAADHI YA WAFANYAKAZI TDL WALIO TEULIWA KWENDA KUTIZAMA KABUMBU UGHAIBUNI
Mweisiga 'Mzee wa jiji' |
Chibehe 'Mzee wa Tanzania' |
Bi Khadija 'Mkuu wa msafara' |
Huyu ndiye Mrema 'Mzee wa Mwanza' |
KAMPUNI ya Tanzania Distilleries Ltd (KONYAGI) imeshinda tuzo ya utendaji bora wa bidhaa (SABMILLER AFRICA MB COMPLEMENTARY BEVERAGE CATEGORY AWARD FOR F 13), ni miongoni mwa Kampuni tanzu za Sabmiller ya Afrika Kusini.
Akiongea na waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Konyagi ya Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa, aliyepambana mpaka kupatikana kwa ushindi huo. amesema kuwa wanajivunia kuwa washindi miongoni mwa makampuni mengi yaliyo chini ya Sabmiller.
“Ushindi huu ni ishara kubwa ya mafanikio KONYAGI na sisi hatutarudi nyuma hii ni chachu katika kutufanya tuendelee kuzalisha bidhaa bora na zenye viwango vya hali ya juu kwa bei nafuu na kuzishinda kampuni zingine” alisema Mgwassa.
Amesema kuwa ushindani ulikuwa mkubwa sana mana kila Kampuni miongoni mwetu inajitahidi kuzalisha bidhaa kwa kiwango cha hali ya juu na sisi kushinda ni ishara kuwa bidhaa zetu zinakubalika kila mahali hapa Africa hata nje ya Africa.
ZAWADI YA KWENDA
Licha ya kupewa tuzo ya ubora, pia TDL imepewa nafasi kwa Wafanyakazi wake watano kwenda kuangalia mpambano mkubwa la ligi kuu ya Hispania (LA LIGA) kati ya Barcelona na Real Madrid.
Mgwassa aliwataja wafanyakazi wanaokwenda Hispania kuangalia mechi hiyo kuwa ni Joseph Chibehe, Khadja Madawili, Bavon Ndumbati, Michael Mrema na Mwesige Mchuruza.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.