ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 23, 2013

SHULE ZENYE MAJINA YA WATU MASHUHURI NCHINI NYINGI ZIKO KATIKA HALI TETE

Ndugu Juma Makongoro akikabidhi Madawati 30 kwa Bw. Madaraka Nyerere ambaye ni moja kati ya wajumbe wa shule ya msingi Ikizu A. Picha na Maktaba ya G. Sengo
Sehemu ya wanafunzi wa shule ya msingi Ikizu A wakiimba katika mahafali ya shule hiyo kwa mwaka huu 2013.
Imekuwa suala la kawaida kwa shule nyingi nchini ambazo zina majina ya watu mbalimbali mashuhuri au zile ambazo walizosoma watu mashuhuri wa taifa hili kuwa katika hali mbaya kimazingira na kukumbwa na uhaba mkubwa wa vitendea  kazi.

Suala hili limeota mizizi na kila kukicha shule nyingi zimekuwa zikiibuliwa suala ambalo limezua maswali mengi moja ni kuu ni Either Mamlaka zinazohusika (Kamati za shule) zinajisahau kuwa viongozi wao wakubwa wametoka shule hizo na kuacha kuzikarabati au viongozi wenyewe kutokujenga mazoea ya kuzitembelea shule zao walizosoma kuona matatizo na changamoto wanazokabiliana nazo.

Katika hilo wadau mbalimbali nchini wakiwemo wafanyabiashara, wanasiasa na watumishi wa sekta mbalimbali hapa nchini wameombwa kuchangia fedha ili kufanikisha ukarabati wa majengo ya darasa yaliyoanguka,kuboresha nyumba za waalimu pamoja na changamoto ya kuweka umeme katika shule ya msingi Ikizu mkoani Mara.

Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Afisa wa Uvuvi Kanda ya Ziwa Juma Makongoro ambaye alikuwa mgeni rasmi wa maafali ya darasa la saba kwa Shule ya Msingi Ikizu A iliyopo wilayani Bunda, kijiji cha Nyamswa mkoani Mara. (MSIKILIZE KWA KUBOFYA PLAY)

Moja kati ya watu mashuhuri waliosoma katika Shule hiyo ni pamoja na  Mwenyekiti wa Tume ya Katiba nchini  Jaji Joseph Sinde Warioba, Brigedia Lyakitimbu, Kanali Wema Chakoma, Watoto wote wa Chief Makongoro. 

HISTORIA Shule ya Ikizu A enzi za ukoloni na kipindi cha miaka ya 80 hadi mwishoni mwa miaka ya 90 inatajwa kuwa ni moja kati ya shule zilizokuwa zikiongoza katika utoaji elimu bora, hali ya mazingira safi kwa kuwa na bustani nzuri zenye maua na miti, maji ya bomba, vyumba vya madarasa vilivyopakwa rangi na vyenye sakafu ya saruji pamoja na mazingira bora yaliyokuwa yakivutia kila mwalimu kutaka kuhamia ili kufundisha shule hiyo lakini leo hali ni tete.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.