HUKU MBAWA ZIKIWA KATIKA MOTION ILEILE YA KUPUNGUZA SPIDI.
IKITUMIA TAIRI ZA NYUMA PEKEE IRIJIBURUZA KWENYE MAJANI TOKEA HAPA MPAKA KULEEE
KAMA INAVYONEKANA.
ABIRIA WAKIHAHA WASIJUE KINACHOENDELEA NA NINI HATMA YA SAFARI YAO KWENYE MLANGO WA UKAGUZI NA UPEKUZI KIWANJANI HAPO.
MOJA KATI YA MIZIGO ILIYOKWAMA KUONDOKA NI PAMOJA NA NDOO ZENYE SAMAKI WA MWANZA ZILIZOKUWA ZIONDOKE NA ABIRIA KUPITIA NDEGE HIYO LEO SAA MBILI NA NUSU ASUBUHI KUELEKEA DAR.
NDEGE YA ATCL BOING 737-200 IKIWA NA WANAANGA 7 NA ABIRIA 39 LEO IMENUSURIKA KUPATA AJALI MBAYA WAKATI IKITUA KATIKA ENEO LA AIR PORT JIJINI MWANZA. CHANZO CHA AJALI HIYO INASEMEKANA KUWA KINATOKANA NA HALI YA HEWA KUWA MBAYA KUTOKANA NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA ZILIZOSABABISHA MAJI KUTUAMA NA KUSABABISHA MADIMBWI MAKUBWA YA MAJI KATIKA BARABARA ZA UWANJA HUO. WAKATI NDEGE HIYO IKITUA ILIKITA MOJA YA MADIMBWI HAYO YA MAJI, MOJA YA INJINI IKAZIMA SAMBAMBA NA TAIRI LA MBELE KUINGIA NDANI KUTOKANA NA MKITO NA KUSABABISHA NDEGE KUJIBURUZA HUKU ILIPOTEZA UELEKEO, KUACHA NJIA YAKE NA KUELEKEA PEMBEZONI MWA BARABARA KWENYE NYASI. KWA KIASI KIKUBWA INJINI YA NDEGE HIYO IMEATHIRIKA NA ITACHUKUA MUDA KWA NDEGE HIYO KUREJEA KIZIGONI. HADI NAKULETEA TAARIFA HII UWANJA WA NDEGE WA MWANZA UMEFUNGWA KWA NDEGE KUBWA KUINGIA MPAKA PALE TAARIFA ZAIDI ZITAKAPOTOLEWA. MBALI NA ABILIA KUKWAMISHWA SAFARI IKIWA NI PAMOJA NA WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA YA UGANDA AMBAO WALIKUWA WAWASILI MAPEMA LEO KWAAJILI YA MCHEZO BAINA YAO NA TAIFA STARS ATHARI NYINGI ZA KIUCHUMI ZIMERIPOTIWA.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.