Eeneo lililoathirika na mlipuko wa bomu Poland
Jeshi la Poland liliwekwa katika hali ya tahadhari siku ya Jumanne jioni baada ya kombora kutua katika eneo lake na kuua watu wawili.
Hatua hiyo ilijiri wakati Urusi iliporusha makumi ya makombora huko Ukraine na vikosi vya Ukraine vilijaribu kuyaangusha kwa makombora yake – ikiwa sehemu ya mfumo wake wa ulinzi wa anga.
Wakati mamlaka ya Poland - pamoja na washirika wa Nato - walipojaribu kubaini ukweli, timu ya uchunguzi ya BBC imekuwa ikichambua ripoti na kusoma picha kwenye mitandao ya kijamii ili kujaribu kufichua maelezo zaidi kuhusu tukio hilo.
Mlipuko huo ulikuwa wapi?
Mlipuko huo uliripotiwa kwa mara ya kwanza kwenye vyombo vya habari vya Poland Jumanne jioni, vikielezea mlipuko karibu na kijiji cha Przewodow, nchini Poland, takriban kilomita 6 kutoka mpaka wa Ukraine.
RIPOTI za awali zilisema kuwa kombora hilo lilitua karibu na eneo la shamba ambalo wafanyikazi hupakia na kupima nafaka, na kuharibu jengo la karibu.
Tulikagua picha za satelaiti (ambazo zilionyesha shamba moja pekee katika kijiji) na kuzirejelea kwa njia tofauti na picha zilizopigwa eneo hilo Jumatano asubuhi ili kupata tovuti - ambayo imethibitishwa na mamlaka ya Poland.
Pia tulikagua video ambayo iliwekwa kwenye mitandao ya kijamii jioni ya Jumanne.
Inadai kuonyesha matokeo ya mara moja ya mlipuko kama kombora "lililoanguka kwenye eneo la Poland". Eeneo linalofuka moshi linaweza kuonekana .
Kuna vidokezo vya kuona kwenye video ambavyo vinafanana na tovuti katika Przewodow.
Mchoro unaoonyesha picha ya skrini ya video na ramani ya eneo karibu na mlipuko
Barabara inayoonekana kwenye video (iliyoangaziwa na sisi kwa rangi nyekundu) ina muundo sawa na ile inayoonekana kwenye picha ya anga ya eneo hilo
Barabara mbele ya jengo la rangi nyepesi (iliyoangaziwa nasi katika machungwa).
Picha zilizopigwa ardhini siku ya Jumatano (zinazoonekana kwenye mchoro wa kwanza) zinaonyesha nyumba ya rangi nyepesi karibu na shamba hilo.
Na mimea na mistari ya miti inaonekana .
Tumejaribu kuwasiliana na mtu aliyechapisha video hii ili kuithibitisha zaidi lakini bado hatujapata jibu.
Picha kutoka kwa tovuti ya mlipuko pia zilianza kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii jioni ya Jumanne, zikionyesha moto na trekta na trela ilioharibika.
Ilikuwa vigumu kupata hizi peke yao kwa sababu ya giza na ukosefu wa dalili pana za kuona.
Lakini picha iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii na polisi wa Poland Jumatano asubuhi inaonyesha maafisa wakichunguza eneo la tukio. Trela , nafaka zilizomwagika na uchafuuinaweza kuonekana kwenye picha zote mbili.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.