Mshambuliaji wa timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kulia akiwani mpira dhidi ya timu ya KCMC wakati wa michuano ya Shimuta inayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja vya Mizani Jijini Tanga
Mshambuliaji wa timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kulia akiwani mpira dhidi ya timu ya KCMC wakati wa michuano ya Shimuta inayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja vya Mizani Jijini Tanga
Na Oscar Assenga,TANGA.
MABINGWA Watetezi wa Michuano ya Shimuta kwa upande wa Mpira wa Miguu miaka miwili mfululizo timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetamba kuendeleza wimbi la kuchukua kombe hilo.
Tambo hizo zilitolewa na Katibu wa timu ya TRA Hamna Shomari mara baada ya kumalizika kwa mechi yao ya mpira wa miguu dhidi ya KCMC ambayo ilimalizika kwa timu hizo kugawana pointi mojamoja baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1.
Mchezo huo ulichezwa kwenye viwanja wa mizani ya zamani Jijini Tanga ambapo timu ya TRA ililazimika kusawadhisha bao lao kipindi cha Pili kupitia Datram Benzema ambaye alitumia uzembe wa mabeki kupachika wavuni bao hilo na hivyo kuamsha shangwe uwanja mzima.
Awali kabla ya timu TRA kuandika bao hilo timu KCMC ndio ilikuwa ikiongoza kufunga bao ambalo lilifungwa na Yusuph Madili aliyepiga faulu ya kona iliyotinga moja kwa moja.
Shomari alisema kwamba wanamshukuru mwenyezi Mungu kwa kuwawezesha kupata Sare na wana mechi nyengine kesho hivyo wana matumaini watarekebisha mapungufu na kufanya vizuri Michezo ijayo.
Alisema kwamba wamepania kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kwenye mechi yao dhidi ya timu ya PSSF.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.