ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 10, 2014

WATU 11 WAUAWA KWA KUCHOMWA MOTO KIGOMA.

 ONYO PICHA ZIFUATAZO ZINATISHA
TUNAOMBA RADHI...


WATU kumi na moja wameuawa kwa kuchomwa na moto wakiwa ndani na nje ya nyumba baada ya wananchi wenye hasira kali kuwatuhumu watu hao kuwa ni washirikina.
Tukio hilo limetokea leo majira ya saa kumi na moja alfajiri mkoani Kigoma baada ya watu hao kuvamiwa na wananchi hao na kuanza kuchomewa nyumba zao moja baada ya nyingine huku wengine licha ya kufanikiwa kutoka ndani ya nyumba hizo zilizokuwa zimetanda moshi mzito, walipokelewa na wananchi hao wavamizi waliokuwa na majani makavu na matairi ya magari na kuanza kuwawasha moto kuwachoma mithili ya kuni. 

Jeshi la Polisi mkoani Kigoma ambalo ndilo chanzo cha habari hii lilifika eneo la tukio majira ya saa kumi na mbili asubuhi ikiwa ni saa moja mara baada ya tukio nakukuta mifupa sanjari na majivu ya miili, huku miili mingine ikifuka moshi na kuendelea kuteketea, miili mingine ikiwa kama ilisulubiwa kwa kupondwa mawe hadi kifo, ile hali waliofanya tukio hilo wakiwa wametokomea pasipojulikana.  
Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo huku likiwasaka kwa udi na uvumba watu waliohusika na kutenda unyama huo ulio kinyume na haki za binadamu.
WITO UMETOLEWA KWA WANANCHI KUEPUKA KABISA MATUKIO YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA KURIPOTI HARAKA PINDI WANAPOHISI DALILI ZA HALI YA UVUNJIFU WA AMANI ZINAPOJITOKEZA AU MATUKIO KAMILI YA MAASI.

By Magege H Athanas

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.