Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Afya na Ustawi wa Jamii Mkoani Mwanza wamezindua Kampeni ya Uzazi Salama ijulikanayo kama "Jiongeze Tuwavushe Salama".
Kampeni hiyo imezinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella ikiwa na kauli mbiu ya "Kila mmoja wetu anao wajibu wa kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi.Maneno basi, sasa vitendo."
Akiongea katika uzinduzi huo Mhe.Mongella amesema vifo hivyo vinaepukika hivyo jamii ina jukumu kwa kuhakikisha inatambua dalili hatarishi na kuwasaidia wazazi na watoto wachanga.
"Katika kuhakikisha kuwa Vifo hivi vinapungua Serikali ya awamu ya tano ya Mhe. Dkt.John Magufuli imejenga vituo vya afya 352 Nchi nzima na kuongeza upatikanaji wa dawa ili kusaidia wazazi na kiwavusha salama," aliaema Mongella.
Naye Katibu Tawala Msaidizi kwa upande wa Afya Dkt.Thomas Rutachunzibwa amesema kampeni hii ina maana kuwa viongozi mbalimbali wakitumika ipasavyo watachangia kumvusha mzazi salama na haipaswi kuachiwa wadau wa afya pekee.
"Swala la vifo bado ni tatizo tusiwaachie wadau wa afya pekee tubadirishe mtazamo kuhusiana na vifo vya wazazi na watoto wachanga kila mdau ana wajibu wa kumvusha mzazi salama," alisema Dkt. Rutachunzibwa.
Aidha Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Christopher Kadio amesisitiza kuhusu Afya ya uzazi na kumtaka kila kiongozi kuwajibika katika kufanikisha Kampeni hii ya kumvusha mzazi salama, hii inaweza kufanyika katika ngazi mbalimbali katika maeneo yetu ya kazi.
"Sisi tuliopo humu ndani tujiulize, umefanya nini katika kupunguza vifo vya wazazi na watoto wachanga hasa katika maeneo tuliyopo?" Alisema Kadio.
Mkoa wa Mwanza ni Mkoa wa nne kutekeleza uzinduzi wa kampeni hii ambayo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan aliizindua Kitaifa mwaka 2018 kwa lengo la kutokomeza kabisa vifo vya akina mama na watoto wachanga kwa kujiongeza na kuwavusha salama.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.