ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, January 25, 2011

AJALI YAUA WANNE MAGU:TISA MAJERUHI.

TAREHE 22 majira ya saa 10:30 jioni. Watu wanne wamefariki dunia na wengine tisa kujeruhiwa katika ajali mbaya ya gari la abiria aina ya Toyota Costa lenye namba za usajiri T386 AMV lililoacha njia na kugonga mtu mmoja aliyekuwa pembezoni mwa barabara eneo la Msola kijiji cha Mwamagigisi wilayani magu, mkoani Mwanza.OCD NYAMAGANA LILIAN MATOLA.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza OCD Lilian Matola amewataja watu hao waliofariki dunia kuwa ni Visent Mashauri (54) mkulima, mkazi wa Nyakaboja Magu, na Ngokoli Eliasi (18) mwanafunzi wa kidato cha kwanza Shule ya Sekondari Busega wilaya ya Magu.

Wengine waliotajwa kufariki kwenye ajali hiyo ni pamoja na Diana Charles (34) mkulima, mkazi wa Nyalipungu Magu, na Magreth Busuma (28) mkazi wa Masanzakona wilayani Magu.

Aidha Kamanda Matola ameongeza kusema kuwa majeruhi watano kati ya tisa walionusurika na ajari hiyo wametoka hospitali ambapo walikuwa wakipatiwa matibabu huku wengine wanne waliosalia wakiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya hiyo na hali zao zikiendelea vizuri

Nae dereva wa gari hilo Deonad Mashauri (26) mchana wa leo amefikishwa mahakamani kujibu shitaka ya kuendesha gari kwa mwendo kasi hata kusababisha ajali hiyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.