NA ALBERT G. SENGO/MWANZA
Katika kuhakikisha inaiunga mkono Serikalini kwenye utoaji huduma bora ya afya kwa kila Mtanzania Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando imeendesha zoezi la upimaji wa afya bure kwa magonjwa mbalimbali haswa yasiyoambukizwa. Akizungumza wakati wa zoezi hilo Mhadhiri wa Chuo cha Afya Bugando(CUHAS) Samson Apolinary amesema kuwa zoezi wanalofanya linalenga haswa magonjwa yasiyoambukizwa huku akiongeza kuwa katika zoezi hilo wamewalenga haswa waendesha boda boda na bajaji kwani ni moja kati ya kundi lililosahaulika. Aidha Apolinary ametoa wito kwa wakazi wa Mwanza kujitokeza kwenda kupima afya zao sambamba na kupatiwa ushauri wa kitaalamu pamoja na matibabu pale inapobidi.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.