NA ALBERT G.SENGO/SPORTS RIPOTI
NGOMA imesoma Gallants Marumo 1-2 Yanga ukiwa ni mchezo wa hatua ya nusu fainali ya pili Kombe la Shirikisho Afrika. Kazi kubwa imefanywa na wachezaji wote wa Yanga wakiongozwa na Nasreddine Nabi ambaye ni Kocha Mkuu. Ni Fiston Mayele alianza kupachika bao la kuongoza kwa Yanga dakika ya 44 kisha ngoma ikapachikwa na Kenned Musonda dakika ya 67. Musonda alimalizia kazi ya Mayele na kufanya Yanga kuwa mbele kwa jumla ya mabao 4-1 kwa kuwa mchezo wa kwanza Uwanja wa Mkapa Yanga ilishinda mabao 2-1. Bao pekee la Marumo iliyokuwa nyumbani limefungwa na Chivaviro dakika ya 90 lakini ni la kufutia machozi tu. Yanga wanatinga hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa ni kazi kubwa kwa wachezaji na benchi la ufundi. Historia imeandikwa, hongereni Yanga, HONGERA TANZANIATupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.