Na Victor Masangu,Kibaha
MWENGE wa Uhuru umeweka jiwe la Msingi katika mradi wa Maji wa Ruvu Stesheni ambao uliibuliwa na wananchi baada ya mradi wa awali kutokidhi mahitaji ya sasa.
Mradi huo ambao unatarajia kukamilika June mwaka huu unatekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Kibaha kwa gharama ya sh.Miln 328.7.
Akitoa taarifa wakati Mwenge wa Uhuru ulipofika katika mradi huo kuweka jiwe la Msingi Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kibaha Mhandis Debora Kanyika amesema mradi huo umehusisha ujenzi wa tenki la maji la lita 50,000 juu ya mnara wa mita 12.
Aidha amesema mradi huo unaendana na kampeni ya Kitaifa ya kusogeza huduma karibu na wananchi ili kumtua mama ndoo kichwani na kwamba kila ndoo ya lita 20 itauzwa kwa sh. 40.
Amesema awali mradi huo ulikuwa unahudumia na unaunganishia wananchi maji nyumbani na kwenye Taasisi na sasa mradi huo umeongeza wanufaika wapya waliokuwa mbali na huduma ya maji.
"Ndugu kiongozi wa Mbio za Mwenge mradi huu ukikamilika utahudumia wananchi kwa miaka 20 ambapo utatoa huduma kwa wananchi hadi kufikia kaya 520 kwa mwaka 2042" amesema.
Mhandisi Debora amesema mradi huo pia unahusisha ujenzi wa vituo sita vya kuchotea maji, nyumba ya mtambo na utandazaji wa mabomba umbali wa km 3.7
Katika hatua nyingine Mwenge wa Uhuru umezindua vyumba vitano vya Madarasa ambavyo vinalwenda kutatua tatizo la.msongamano uliotokana na ongezeko la wanafunzi kutokana na sera ya elimu bila Malipo
Mwenge wa Uhuru umepitia miradi 14 yenye thamani ya sh. Trillion 3.1kati ya fedha hizo sh. Miln 193.5 mchango wa Halmashauri, sh. Biln 5.9 kutoka Serikali kuu na Trilion 3.1 nguvu za wananchi na michango ya mwenge ni sh. Miln 3.1.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa 2023 Abdallah Shaib amepongeza miradi ya utunzaji wa mazingira inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo ikiwemo upandaji miti unaoendelea kwenye Taasisi na maeneo mbalimbali.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.