Mwanamke mwenye umri wa miaka 26, ambaye alinaswa kwenye video akimlisha mtoto wake wa kambo mwenye umri wa miaka 4, kinyesi amekamatwa
Kwa mujibu
wa ripoti iliyotolewa na polisi nchini Uganda Jumatatu, Mei 15, mwanamke huyo
anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Jinja ambapo kesi ya kuteswa na
unyanyasaji wa watoto ilifunguliwa dhidi yake.
Video hiyo
ambayo tarehe yake ya kurekodiwa haijulikani, inamuonyesha mwanamke huyo ambaye
polisi wamemtambua kwa jina la Esther Nabirye, akimlazimisha mtoto huyo kula
kinyesi chake baada ya kudaiwa kujisaidia haja kubwa kwenye sebule.
Msemaji wa
polisi, Fred Enanga alitaja vitendo vya Nabirye kuwa vya kinyama na visivyo vya
kibinadamu.
Polisi
walisema mvulana huyo atapelekwa kwenye makazi ya dharura ya watoto
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.