ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, May 15, 2024

RPC PWANI AZINDUA KITUO CHA PYRAMID OIL KIBAHA AWAPA SOMO BODA BODA KUTII SHERIA

 


NA VICTOR MASANGU,KIBAHA 

JESHI la Polisi Mkoa  Pwani limewaonya  vikali baadhi ya  madereva wa Bodaboda kuacha kabisa na kuingilia misafara ya viongozi waandamizi na badala yake wanapaswa kuiheshumu pindi inapopita ili kuweza kuepukana na ajali ambazo zinaweza kupelekea watu kujeruhiwa vibaya na kupoteza maisha yao.

Onyo hilo  limetolewa na Kamanda wa Polisi mkoani Pwani  Pius Lutumo wakati Jeshi la Polisi  kwa kushirikiana na Kampuni ya Priamid oil walipotoa Elimu ya usalama barabarani sambamba na  uzinduzi rasmi  wa kituo ha mafuta  kilichopo eneo la kwa Mbonde  mkoani Pwani


Kamanda Lutumo alisema kwamba madereva wa boda boda wanapaswa kuweka misingi ya kuheshimu misafara ya viongozi waandamizi ikiwa sambamba na kuzingatia sheria mbali mbali za barabarani.

Aidha Kamanda Lutumo aliwapongeza wawekezaji wa kiwanda hicho cha Pyramid Oil kwa kuamua kukijenga katika eneo la Kibaha ambalo kwa sasa lina viwanda mbali mbali ni moja ya hatua ya kuleta chachu ya maendeleo.


Kwa upande Kaimu Mkuu wa kikosi cha  Usalama Barabarani Mkoa wa Pwani Miraj Mkojera amewataka bodaboda hao kuachana kabisa  na tabia ya kubeba mishikaki na kuwahimiza kuvaa kofia  ngumu ili kujilinda pindi ajali inapotokea.

Naye mmoja wa wawekezaji ambaye pia ni mkurugenzi wa kituo hicho cha mafuta cha Piramid Victor  Betram amempongeza Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwawekea mazingira mazuri ya uwekezaji.

Mkurugenzi huyo alifafanua kwamba uwezezaji huo wa kituo cha mafuta umeweza kuwapa fursa mbali mbali za ajira kwa wakazi kutoka Wilaya ya  Kibaha kwa kiwango cha asilimia mia moja.

Pia Mkurugenzi huyo alibainisha kwamba kituo hicho ambacho kimefunguliwa rasmi kimeshatoa fursa za ajira zaidi ya 15 na kwamba kitaendelea kutoa ajira kadiri ya mahitaji.

Nao baadhi ya madereva wa  bodaboda ambao wamehudhuria katika halfa hiyo wameahidi kutekeleza maagizo na maelekezo yote ambayo yametolewa na jeshi la Polisi.

Kadhalika walisema ujio wa mradi huo wa kituo cha mafuta utaweza kuwasaidia kuondokana na kwenda kutafuta huduma ya mafuta katika eneo la mbali na kudai  kwao ni mkombozi mkubwa.

Katika halfa ya uzinduzi rasmi wa kituo hicho cha mafuta pia kulitolewa mafunzo mbali mbali kwa madereva wa boda boda kutoka kwa jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani lengo ikiwa ni kuwakumbusha kuzingatia sheria za barabarani bila kushurutishwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.