ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, May 13, 2024

JAMAA ALIYEPANDIKIZWA FIGO YA KWANZA YA NGURUWE AFARIKI DUNIA

 


Mwanamume wa kwanza kupandikizwa figo ya nguruwe iliyobadilishwa vinasaba amefariki miezi miwili baada ya upasuaji huo, hospitali iliyotekeleza utaratibu huo imesema.

Richard "Rick" Slayman, 62, alikuwa akiugua ugonjwa wa figo hatua ya mwisho kabla ya kufanyiwa upasuaji huo mnamo mwezi Machi.

Hospitali kuu ya Massachusetts (MGH) ilisema Jumapili hakuna dalili kwamba kifo chake kilikuwa matokeo ya upandikizaji.

Upandikizaji wa viungo vingine kutoka kwa nguruwe waliobadilishwa vinasaba haukufaulu hapo awali, lakini operesheni dhidi ya Bw Slayman ilisifiwa kuwa hatua muhimu ya kihistoria.

Mbali na ugonjwa wa figo, Bw Slayman pia aliugua kisukari cha Aina ya 2 na shinikizo la damu. Mnamo 2018, alipandikizwa figo ya binadamu, lakini ilianza kushindwa kufanya kazi baada ya miaka mitano.

Kufuatia upandikizaji wa figo yake ya nguruwe mnamo Machi 16, madaktari wake walithibitisha kuwa hahitaji tena dayalisisi baada ya kiungo hicho kipya kusemekana kufanya kazi vizuri.

"Bw Slayman ataonekana milele kama mwanga wa matumaini kwa wagonjwa wengi wa upandikizaji duniani kote na tunamshukuru sana kwa imani yake na nia yake ya kuendeleza uwanja wa upandikizaji wa xeno," ilisema taarifa ya MGH.

Xenotransplantation ni kupandikiza seli hai, tishu au viungo kutoka kwa spishi moja hadi nyingine.

MGH ilisema "imehuzunishwa sana" na kifo chake cha ghafla na kutoa rambirambi kwa familia yake.

Jamaa wa Bw Slayman walisema simulizi yake ilikuwa ya kutia moyo.

“Rick alisema kuwa moja ya sababu zilizomfanya afanyiwe utaratibu huu ni kutoa matumaini kwa maelfu ya watu wanaohitaji upandikizaji kuishi,” walisema.

"Rick alitimiza lengo hilo na matumaini yake yatadumu milele.

"Kwetu sisi, Rick alikuwa mtu mwenye moyo mkunjufu na mcheshi ambaye alijitolea sana kwa familia yake, marafiki, na wafanyikazi wenzake," waliongeza.

Ingawa Bw Slayman alipokea figo ya kwanza ya nguruwe kupandikizwa kwa binadamu, sio kiungo

Wagonjwa wengine wawili wamepandikizwa moyo wa nguruwe, lakini taratibu hizo hazikufua dafu kwani waliopokea huduma hiyo na kufariki wiki chache baadaye.

Katika kesi moja, kulikuwa na ishara kwamba mfumo wa kinga ya mgonjwa ulikuwa umekataa kiungo, ambayo ni hatari ya kawaida katika upandikizaji.

CHANZO:- BBC SWAHILI

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.