ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, August 20, 2019

WAANDISHI WA HABARI MTANDAONI 'BLOGS & ONLINE TV' WAPIGWA MSASA KUHUSU HAKI ZA BINADAMU

Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media -  Blogs/ Online TV) nchini wametakiwa kujitafakari na kutimiza wajibu wao katika utetezi wa haki za binadamu.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumanne Agosti 20,2019 na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC) Claud Gwandu wakati akifungua mafunzo ya Haki za Binadamu Jijini Dodoma yanayoratibiwa na Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kupitia ya Klabu Waandishi wa Habari mkoani Arusha (APC) kwa ufadhili wa Mfuko wa Maendeleo wa Watu wa Marekani kupitia taasisi za Freedom House pamoja na PACT.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC) Claud Gwandu wakati akifungua mafunzo ya Haki za Binadamu mjini Dodoma yaliyoshirikisha waandishi wa habari mtandaoni (Blogs/Online Tv ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) kupitia vyombo vya habari mbadala (Alternative Media)
 Gwandu alisema ni vyema waandishi wa habari wa vyombo vya habari wakatumia mafunzo wanayopewa na kuonesha kwa vitendo namna gani mafunzo ambayo wamekuwa wakipewa yanawasaidia katika kazi zao.

"Washiriki wa Work Group Three inayohusisha waandishi wa habari mtandaoni tutimize wajibu wetu kwa yaliyo ndani ya uwezo wetu, bado hatujaona habari za haki za binadamu na demokrasia kama ambavyo tunatakiwa kufanya",alisema.

"Tunaendelea kufuatilia kwa makini namna gani tutapunguza washiriki katika kundi hili, wafadhili wetu wameendelea kujiuliza na kuhoji kuhusu mafunzo tunayopewa na wajibu wetu",

"Nyinyi ni watu wazima mjitathimini mmesafiri kutoka kwenu kuja kushiriki mafunzo yanayogharamiwa kwa fedha nyingi,halafu hatuoni mabadiliko makubwa,hatutasita kupunguza washiriki ili tubaki na wale wanaozingatia kinachofundishwa",aliongeza Gwandu.
 Naye Mwezeshaji wa mafunzo hayo Wakili Froldius Mutungi akizungumzia kuhusu haki alisema, haki za binadamu hazirithiwi wala kutolewa na mtu hivyo ni wajibu wa waandishi wa habari wana jukumu kubwa la kulinda haki za binadamu na kupaza sauti pale haki zinapovunjwa.

Mafunzo hayo ya Haki za Binadamu ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) kupitia vyombo vya habari mbadala (Alternative Media).
Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.