ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, August 19, 2019

LAKAIRO INVESTMENT CO. LTD FUNGA FUNGUA MWAKA 2019


KATIKA kuchochea ari ya uchapakazi kwa maksudi ya kufikia Uchumi wa Viwanda wenye tija Wafanyakazi wa Lakairo Investment Company Limited, kutoka katika viwanda wazalishaji wa bidhaa mbalimbali jijini hapa wamefanya sherehe za funga & fungua mwaka zilizofanyika katika hotel ya ufukweni mwa ziwa Victoria ijulikanayo kama Bugando Beach, Nyanguge wilayani Magu.

Sherehe hizo zilizofana zimeambatana na kongamano la kujadili na kutathimini shughuli za utendaji sanjari na changamoto za wafanyakazi na viongozi.

 Akizungumza wakati wa sherehe hizo Mkurugenzi Mkuu wa Lakairo Investment Company Limited, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rorya  Lameck Airo amewapongeza wafanyakazi wote kwa ubunifu na uchapakazi waliouonyesha katika kampuni hiyo kiasi cha kuwa moja ya chachu ya mafanikio na maendeleo yanayoonekana sasa na kuwasihi kuzingatia maadili ili waweze kufikia malengo ya kampuni na wao kunufaika.Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.