Shamba la Mifugo la Mabuki lililopo wilayani Misungwi mkoani Mwanza lilianzishwa mnamo mwaka 1966 baada ya Uhuru wa Tanganyika kwa ajili ya kuzalisha F1, hii ilikuja baada ya kugundua kuwa wafugaji wachache waliopewa ng’ombe wa kisasa kutoka Ulaya, wengi wao walishindwa kuwamudu wakafa ndipo wataalamu wa Mifugo waliokuwepo enzi hizo wakaona ni vyema kuzalisha ng’ombe wa maziwa wanaoweza kuhimili mazingira ya nyanda za nchi zenye joto ikiwemo Tanzania.
Shuhudia ziara ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina akizuru Shamba hilo la Mabuki kama sehemu ya mwendelezo wa Agenda ya Kitaifa ya Utafiti wa Mifugo, Uvuvi na Ukuzaji viumbe kwenye maji 2020 – 2025 ambapo pia amepata fursa ya kuwaona Nyati Maji wanaofugwa kituoni hapo, mbegu iliyoingizwa nchini enzi za utawala wa Rais wa Kwanza nchini Hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere. Kwa wale wanaotaka kufuga Nyati hao, kitambo sana Serikali ilishafungua milango.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina.
Pia shamba la Mifugo la mabuki linafuga Mbuzi wa maziwa (hawapo pichani) aina ya Toggenburg wenye uwezo wa kutoa kati ya lita moja na nusu kwa mkamuo mmoja yaani lita 3 kwa siku, kiwango kinachozidi uwezo wa ngombe wa kienyeji anayekamuliwa lita 1 kwa mkamuo na lita 2 kwa siku.
Ng'ombe hasa madume yananunuliwa kwa wingi sana na wafugaji kwaajili ya mbegu.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina akipata maelekezo toka kwa Meneja Msaidizi wa Shamba la mifugo la Mabuki ambaye pia ni Afisa Mifugo Daraja la Kwanza Pascal Godwin Bahemu (mwenye kofia).
Shamba la Mifugo la Mabuki lililopo wilayani Misungwi mkoani Mwanza, lina ukubwa wa Hekta 9,773, ambapo mpaka hivi sasa shamba linauwezo wa kuzalisha ng'ombe 580 kwa mwaka yaani wastani wa 320 majike na 260 madume.
TAFITI ZA AWALI. Kwa tafiti za URT za Mwaka 2015, Tanzania inashika nafasi ya pili kwa wingi wa mifugo barani Afrika ikiwa na ng'ombe milioni 25, mbuzi milioni 16.7, kondoo milioni 8, nguruwe milioni 2.4, na kuku milioni 36. Kati ya ng'ombe milioni 25 ng'ombe wa asili ni 98%. Hivyo, ni 2% tu ya ng'ombe wote Tanzania wanaofugwa kwa mfumo wa ufugaji wa kisasa. Tafiti hizo zinaonesha kuwa ufugaji wa asili unachangia 7.4% ya pato la Taifa na ongezeko la ukuaji la 2.2% kila mwaka. Ufugaji wa asili umethibitika kiuchumi kuwa na ufanisi mkubwa katika matumizi ya ardhi na uhifadhi wa mazingira. Ufugaji wa asili unategemewa na idadi kubwa ya Watanzania kwa kuendesha maisha yao; iwe kwa chakula, mavazi, na maendeleo kwa mapana yake. Mchango wake katika uchumi rasmi na usio rasmi (informal and formal economies) ni dhahiri hasa kupitia kodi na tozo mbalimbali katika masoko ya mifugo, usafirishaji wa mifugo, ukaguzi wa mifugo, na upatikanaji wa malighafi kwa matumizi ya viwanda mbalimbali.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.