MKUTANO wa 19 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeahirishwa leo asubuhi baada ya kujitokeza vurugu;-Mswadaa wa dharura wa Kuundwa Tume Huru ya Uchaguzi ambao uliombwa ujadiliwe katika buge lijalo la 20 ndiyo uliozua yote.
Wakati mtoa hoja wa serikali akiwasilisha hoja ya dharura, Upande wa upinzani waukapinga lakini Spika akapeta.
Ndipo Mnyika akaja na hoja ya kutaka kujadiliwa kwa suala la uandikishaji wa wapiga kura na hatima ya kura ya maoni na kuomba jibu litolewe leo kwa sababu Waziri Mkuu yupo.
Spika akasema hoja yake na ya kwanza zinafanana. Kambi ya Upinzani ikagoma, Spika akawaambia watoke ili bunge liendelee na shughuli zake huku akitoa ahadi kuwa waziri mkuu atatoa majibu baadaye.
Wapinzani wakachachama na kusema hawatoki wakaanza kuimba na kupiga kelele, hapo ikamlazimu spika kuahirisha bunge mpaka baadaye hakusema muda.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.