ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, August 9, 2018

KUKAMATWA KWA MWANDISHI WA HABARI TARIME : OJADACT YAOMBA WAANDISHI KUKUTANA NA SIRROGSENGOtV

OJADACT YASIKITISHWA   NA KITENDO CHA JESHI LA POLISI KUMSHIKILIA MWANDISHI WA TANZANIA DAIMA SITTA TUMMA.

Chama Cha Waandishi wa Habari  wa Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania..(OJADACT), kimeshitushwa na taarifa ya kukamatwa kwa Mwandishi wa Habari Sitta Tumma, anayeandikia Gazeti la Tanzania Daima.


Tumma alikamatwa kwenye mkutano wa siasa wa chama cha CHADEMA hapo Jana Agosti 8, alipokuwa akitekeleza majukumu yake ya kutafuta taarifa km ilivyoainishwa kwenye ibara ya 18 ya KJM na sheria ya haki ya kupata taarifa 2015.

OJADACT , inatambua kuwa, mkutano ya siasa ipo kisheria kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 na kanuni zake za usajili wa vyama vya siasa, uwepo wa mwandishi kwenye tukio pia upo kisheria kwa mujibu wa ibara ya 18 ya katiba, ambayo ndiyo sheria mama ya Nchi.

Mwandishi aliyekamatwa pia alikuwa na kitambulisho cha kumtambukisha kuwa, yeye ni Mwandishi wa habari.

Lakini licha ya kujieleza bado alishikiliwa na kulala kituo cha polisi, na kumsababishia usumbuvu usiokuwa na faida kwa jamii.

OJADACT, tumesikitishwa saba na tukio hilo linalokiuka misingi ya haki za binadamu na sheria za mbalimbali za Nchi na pia kuwa na sura ya kuminya Uhuru wa vyombo vya habari Tanzania.

Chombo cha habari kina dhima kubwa ya kuhabarisha, kuelimisha, kuburudisha na dhima ya kisasa ya kukosoa kwa upande chanya na hasi.

Tunaliomba Jeshi la polisi Nchini, kupitia kwa RPC wa Tarime na Rorya na IGP kuliingilia kati suala hilo na kuhakikisha Mwandishi Sitta Tumma anaachiwa huru, ili aendelee na majukumu yake ya kikazi.

Pia OJADACT inasisitiza vyombo vya habari kuwaandalia Waandishi wake vikoti maalumu press jackets zinazowatambukisha kwa urahisi Waandishi wawepo eneo hatarishi la kutafuta habari.

Tuna imani Sitta Tumma ataachiwa huru kwa kupewa dhamana, kwa kuwa,dhamana ni haki ya msingi km ilivyoaninishwa kwenye sheria ya makosa ya mwenendo wa jinai (CPA).

 EDWIN SOKO 
 MWENYEKITI 
 OJADACT
 9/8/2018

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.