ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 11, 2018

MISHAHARA DUNI KWA MAASKARI WA BAADHI YA MAKAMPUNI BINAFSI CHANZO CHA UHALIFU NCHINI.




GSENGOtV

IMETAJWA kuwa huenda ongezeko la wahalifu wa uvunjaji na wizi wa maeneo kadhaa yenye mali nchini linachangiwa na ukwasi wa maisha wanayoishi baadhi ya walinzi wanaopewa dhamana ya kulinda maeneo mbalimbali ya huduma, majumbani na maeneo ya biashara.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela amefunguka hayo wakati akishiriki hafla ya ufunguzi wa kampuni mpya ya ulinzi ya “Power Shield Security Services Ltd” yenye ofisi zake barabara ya Bugando jijini hapa.
"Matatizo ya ukosefu wa mafunzo, Mishahara midogo, Ucheleweshwaji wa malipo ya mishahara, kutopata mahitaji muhimu na maslahi bora ni moja kati ya sababu zinazo wasukuma baadhi ya walinzi hao wanao pewa dhamana ya kulinda hasa maeneo nyeti yenye thamani na mali kujihusisha na vitendo vya uhalifu" alisema Mongella.

Wakati sekta ya ulinzi binafsi ikiendelea kukua katika miongo michache iliyopita, nayo mifumo iliyopo ya  kudhibiti wahalifu imeendelea kuboreshwa.

Ili kupambana na changamoto hizo  Uongozi wa kampuni mpya ya ulinzi ya “Power Shield Security Services Ltd” iliyozinduliwa Tarehe 10 Agasti 2018 Jijini Mwanza, umeahidi kuimarisha hali ya ulinzi na usalama kwa kutumia askari wake wenye weledi wa hali ya juu pamoja na vifaa vya kisasa ikiwemo kamera.

Ujuzi wa walinzi wake katika kutoa huduma ya kwanza pamoja na huduma ya zimamoto iwapo majanga hayo yanapoweza kujitokeza ni moja kati ya sifa nyinyine za ziada walizonazo watoa huduma kutoka kampuni hilo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.