ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 11, 2016

WATATU WAFA KWA KUFUNIKWA NA KIFUSI GEITA.


Watu watano wamepoteza  maisha na wengine watatu kujeruhiwa vibaya kwa kuvunjika viungo vyao baada ya kufukiwa na kifusi wakati wakichimba mawe yanayodhaniwa kuwa ni dhahabu.

Tukio hilo limetokea juzi saa 9:00 Alasiri, katika kata ya  Mgusu Wilayani Geita  ambapo watu  hao waliangukiwa na ukuta wa udongo waliokuwa wakiuchimba.

Pamoja na tukio hilo la kusikitisha wachimbaji hao wakatoa kilio chao kwa Serikali kuhusu maeneo ya kuchimba yaliyo salama ikiwa ni pamoja na kuwapa zana za kuchimbia na uokoaji.

Katibu tawala ya wilaya ya Geita Gaspar Kanyaiita aliyetembelea eneo hilo ameagiza Ofisi ya Madini kuwakamata wachimbaji wote wanaokiuka kanuni huku kaimu Afisa Madini Mkoa wa Geita akisema eneo hilo limefungwa tangu jana mpaka itapotangazwa utaratibu mwingine.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.