Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amewaonya watu aliosema wanafanya njama za kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa mwezi Agosti mwaka huu.
Rais Kenyatta amewaambia waandishi
wa habari kwamba, hatovumilia kitendo chochote cha kuchochea machafuko
na kwamba sheria itamuadhibu vikali mtu yeyote atakayochochea machafuko
na kujaribu kuvuruga uchaguzi huo.
Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika
tarehe 8 Agosti mwaka huu nchini Kenya. Ikumbukwe kuwa nchi hiyo
ilishuhudia machafuko mabaya ya umwagaji wa damu baada ya uchaguzi mkuu
wa tarehe 27 Disemba 2007. Mamia ya watu waliuawa na wengine wengine
kupoteza makazi yao katika machafuko hayo.
Viongozi wa muungano wa NASA nchini Kenya.
Viongozi wa muungano wa NASA nchini Kenya.
Hivi sasa pia hali ya uchaguzi nchini
Kenya ni ya wasiwasi kiasi kwamba machafuko yamekuwa yakiripotiwa katika
chaguzi za michujo ya wagombea za vyama vya kisiasa nchini humo.
Aidha, hadi hivi sasa muungano wa
upinzani wa NASA umeshindwa kutangaza mgombea wao kutokana na kila chama
kutaka mkuu wake ateuliwe kugombea urais, suala ambalo linazidisha homa
ya uchaguzi nchini humo. Karibu Wakenya milioni 19 wametimiza masharti
ya kupiga kura.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.