Wapinzani wawili wakuu wa Rais Robert Mugabe
wa Zimbabwe wamesema wameamua kuungana ili kuhakikisha kiongozi huyo
mwenye umri wa miaka 93 haendelei kubaki tena madarakani kwa muhula
mwengine wa miaka mitano.
Morgan
Tsvangirai, kiongozi wa chama cha MDC-T ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa
serikali tete ya mseto iliyoongozwa na Rais Mugabe kuanzia mwaka 2009
hadi 2013 amesema yeye na Bi Joice Mujuru, ambaye alikuwa Makamu wa Rais
wa Mugabe hadi alipotimuliwa mwaka 2014, watapigania kuunda serikali ya
mseto ili kuleta mabadiliko ya kisiasa nchini humo.
"Huu ni
mwanzo tu wa kuweka msingi kuelekea uundaji wa muungano mpana zaidi wa
kupambana na ZANU PF kuanzia sasa hadi uchaguzi ujao mwaka 2018",
ameeleza Tsvangirai akikusudia chama tawala kinachoongozwa na kiongozi
huyo mzee zaidi kiumri barani Afrika.
Chama hicho tawala nchini Zimbabwe ambacho kinaiongoza nchi hiyo
tangu ipate uhuru wake mwaka 1980, mwezi Desemba mwaka jana kilimpitisha
rasmi Mugabe kuwa mgombea wake wa urais katika uchaguzi unaotazamiwa
kufanyika katikakati ya mwaka ujao ambapo kiongozi huyo atakuwa
ametimiza umri wa miaka 94.
Bi Majuru
ambaye mwaka jana aliunda chama kipya cha Taifa cha Wananchi amesema
vyama vyao viwili vya upinzani vimekuwa vikijadiliana kwa muda wa miezi
sita ili kufikia makubaliano na kwamba sasa wanatarajia kuanza
mazungumzo ya kina juu ya masuala maalumu ili kuimarisha muungano wao.
Wapinzani
wanamlaumu Rais Mugabe kwa kuua uchumi wa Zimbabwe ambayo ni moja ya
nchi za Kiafrika iliyokuwa na ustawi mkubwa; hata hivyo chama chake
kinasema uchumi wa nchi hiyo umedhoofishwa na madola ya Magharibi
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.