NA ANNASTAZIA MAGINGA, Mwanza
TIMU ya mpira ya Pamoja Sport Club imeingia mitini kwa kushindwa kuonekana kwenye mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 15
yanayoendelea kwenye uwanja wa Nyamagana kwa ajili ya kuibua vipaji vya vijana
hao
Mashindano yaliyoandaliwa na Chama cha Mpira wa miguu Wilaya
ya Nyamagana kwa ajili ya kuibua vipaji vya vijana wenye umri chini ya miaka 15
ili kuhakikisha wanafanya vizuri katika soka hapo baadae
.
Akizungumza na Gsengo blog Mwenyekiti wa Mashindano hayo
Selemani Makasi amesema timu hiyo imeshindwa kuhudhuria leo kwenye mechi hiyo
baada ya kuwaondoa vijana watatu hapo
jana waliokuwa wamezidi umri hatua iliyopelekea kutoleta timu yao leo kwa ajili
ya kuendelea na mashindano hayo.
“Changamoto tulionayo katika kuibua vipaji kwa watoto ni umri wa miaka 15,timu nyingi zinazoshirki
mashindano haya zinalenga ushindi tu lakini lengo letu ni kuibua vipaji,sasa
kilichotokea kwa timu ya pamoja ni baada ya jana kuwaondoa vijana wao 3
waliozidi umri wameamua kuzila
mashindano”amesema Makasi.
Amesema Viongozi pamoja na makocha wa timu hizo wanatakiwa
kuwa wa kweli kwani mashindano yanalenga kuibua vipaji na kuleta soka lenye
ubora kwa watoto.
Timu ya Pamoja Sport Club ilitakiwa kuchuana leo na Alliance kwenye
uwanja huo hatua iliyowafanya wapinzani wao kujizolea pointi tatu baada ya kushindwa
kuonekana.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.