|
Afisa Tawala wilayani Nyamagana, Zubeda Kimaro (mbele), akizindua
ofisi ya Sun King Jijini Mwanza ikiwa ni uzinduzi rasmi wa kampuni hiyo
kitaifa hii leo. Kulia ni Mkuu wa Masoko wa kampuni ya Sun King
Tanzania, Judie Wu. |
|
Meneja Masoko wa kampuni ya Sun King nchini Tanzania, Albert Msengezi, akizungumza na wanahabari kwenye uzinduzi rasmi wa ofisi na bidhaa za Sun King nchini, uliofanyika hii leo Buzuruga Plaza Jijini Mwanza.
|
|
Mgeni Rasmi, Afisa Tawala wilaya ya
Nyamagana mkoani Mwanza, Zubeda Kimaro, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa
Mkoa wa Mwanza, John Mongella, kwenye uzinduzi rasmi wa ofisi na bidhaa
za Sun King nchini Tanzania, uliofanyika Buzuruga Plaza Jijini Mwanza
hii leo. |
|
Mkuu wa Masoko wa kampuni ya Sun King Tanzania, Judie Wu, akizungumza na wandishi wa habari kwa maswali ya ufafanuzi kupitia kusanyiko la uzinduzi rasmi wa ofisi na bidhaa za Sun King nchini Tanzania, uliofanyika Buzuruga Plaza Jijini Mwanza hii leo.
|
|
Wadau mbalimbali katika kusanyiko la uzinduzi rasmi wa ofisi na bidhaa za Sun King nchini Tanzania, uliofanyika Buzuruga Plaza Jijini Mwanza hii leo. |
|
Mstari wa mbele kusanyiko la uzinduzi rasmi wa ofisi na bidhaa za Sun King nchini Tanzania, uliofanyika Buzuruga Plaza Jijini Mwanza hii leo. |
|
Kwa umakini kuzingatia yaliyomo. |
|
Sun King. |
|
Kwa umakiini zaidi. |
|
Kusanyikoni. |
|
Mbele ya mjengo uliopo Buzuruga Plaza Mwanza. |
|
Meneja Masoko wa kampuni ya Sun King nchini Tanzania, Albert Msengezi,akifunguka juu ya faida na matumizi ya taa za sola. |
|
Afisa Tawala wilayani Nyamagana, Zubeda Kimaro (mwenye kofia) akipokea maelezo kuhusu faida na uimara wa baadhi ya taa za Sun King kupitia jumba la ofisi ya Sun King Jijini Mwanza ikiwa ni uzinduzi rasmi wa kampuni hiyo
kitaifa hii leo, kushoto mtoa maelezo ni Mkuu wa Masoko wa kampuni ya Sun King
Tanzania, Judie Wu. |
Wakazi wa
maeneo ambayo bado hayajafikiwa na huduma ya umeme nchini, wanatarajiwa
kunufaika na huduma hiyo kupitia mitambo ya umeme wa jua kwa bei nafuu
inayosambazwa na kampuni ya Sun King.
Meneja Masoko
wa kampuni hiyo nchini, Albert Msengezi, ameyabainisha hayo hii leo
Jijini Mwanza kwenye uzinduzi rasmi kitaifa wa bidhaa za Sun King ambazo
ni taa za sola pamoja na majiko bunifu ya Jikokoa.
“Kila Kijiji
nchini tunakusudia kuwa na mawakala wa kampuni ya Sun King ambao
watawafikia wananchi wote wanaoishi katika maeneo hayo na hadi kufikia
mwishoni mwa mwaka huu tunakusudia kuwa na wanufaika zaidi ya Milioni
Moja ambapo tumejikita kwenye bidhaa bora zisizochafua mazingira ikiwemo
taa za sola na majiko yasiyochafua mazingira”. Amebainisha Msengezi.
Mkuu wa Masoko
wa kampuni ya Sun King, Judie Wu, amesema kampuni hiyo imedhamiria
kuhakikisha kila mmoja Mjini na Vijijini anapata huduma ya umeme pamoja
na kutumia majiko bunifu yasiyo na madhara kiafiya kwa bei nafuu.
Akizungumza kwa
niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwenye uzinduzi huo wa bidhaa za King
Sung, Zubeda Kimaro ambaye ni Afisa Tawala wilayani Nyamagana,
amewahimiza wawekezaji kujitokeza kwa wingi kuwekeza mkoani Mwanza kwani
kuna fursa nyingi za kiuwekezaji hatua ambayo pia itazalisha ajira
zaidi kwa vijana.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.