NA ALBERT G. SENGO
MWANZA Casino pamoja na klabu maarufu ya burudani ijulikanayo kwa jina la Club Dallas iliyoko katika jengo ya Mwanza Hotel jijini Mwanza vimeteketea kwa moto Jumatano ya tarehe 31 Agosti 2022 kuanzia majira ya saa 1 hadi majira ya saa 4 na dakika kadhaa usiku, huku chanzo cha moto huo kikiwa hakijajulikana. Jicho la camera ya @jembefmtz limekuwashuhuda kwenye eneo hilo likishuhudia baadhi ya maofisa wa Jeshi la cha Zimamoto na Uokoaji wakihaha wakifanya jitihada za kuuzima moto huo ambao ulikuwa na tabia ya kuzimika na kuwaka.Baadhi ya magari yaliyokuwa yamepaki karibu na eneo hilo la hoteli yaliamuliwa kuondolewa haraka, nalo jeshi la polisi likidhibiti wananchi kusogea karibu na eneo la tukio kwa sababu za kiusalama. Adam Malima ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na hapa anazungumza..... Bado hakuna taarifa za madhara kwa binadamu zilizoripotiwa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.