ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, October 26, 2010

TIGO YAZINDUA TAWI JINGINE MWANZA.

MKUU MPYA WA WILAYA YA NYAMAGANA MH. SAID ALLI AMANZI AKIFUNGUA RASMI OFISI MPYA ZA TIGO JENGO LA CBE MWANZA.

MGENI RASMI ALITOA PONGEZI TIGO KWA KUTUNUKIWA TUZO YA BIDHAA BORA KWA KAMPUNI ZA MAWASILIANO NCHINI NA WATAALAM WA SUPERBRAND, PIA KWA KUTOA MAWASILIANO KWA GHARAMA NAFUU KWA WATANZANIA WOTE SAMBAMBA NA KUTOA AJIRA KWA VIJANA.

TIGO SASA IMETIMIZA JUMLA YA MATAWI 26 NCHI NZIMA, MWANZA IKIWA NA MATAWI MAWILI. PICHANI NI TECHNICAL MANAGER BW. BERNARD.

MGENI RASMI AKITEMBEZWA NDANI YA OFISI HIZO MPYA KUJIONEA BIDHAA MBALIMBALI ZA TIGO.

KATIKA TAWI HILI KUNA IDARA YA HUDAMA KWA WATEJA YENYE WAFANYAKAZI WAPATAO SITA. IDARA YA MASOKO NA USAMBAZAJI YENYE WAFANYAKAZI WAPATAO 12 PAMOJA NA TIMU YA MAUZO YA WATU 200.

ZAWADI KWA MKUU WA WILAYA YA NYAMAGANA KUTOKA TAWI JIPYA LA TIGO LILILOPO JENGO LA CBE MWANZA.

KUTOKANA NA MVUTO WA SIMU MPYA TOKA TIGO AMBAZO ZIKO KWENYE PROMO HIVI SASA, MGENI RASMI ALIAMUA KUMNUNULIA MKEWE MOJA YA SIMU HIZO NA HAKUSITA KUTAMKA WAZIWAZI.

PICHA YA PAMOJA WAFANYAKAZI WA TIGO TAWI HILO JIPYA NA MGENI RASMI MKUU WA WILAYA YA NYAMAGANA MH. SAIDI ALLI AMANZI.

WADAU WA TIGO NA VIPEPERUSHI VYA HUDUMA KWA WATEJA.

TIGO WANASEMA BURUDANI MUHIMU KUKOSHA MACHO.
TIGO IMEAHIDI KUENDELEZA KANUNI YAKE YA KURAHISISHA MAWASILIANO HUKU IKIMWAGA MAAJABU MTAANI.

HUDUMA ZITOLEWAZO NI PAMOJA NA KURUDISHIWA LAINI ILIYOPOTEA, USAJIRI WA NAMBA ZA SIMU, HUDUMA YA TIGO PESA, KUTENGENEZA LAINI MPYA, KUPATA HUDUMA YA INTANET, KUPATA HUDUMA YA NYIMBO KWENYE SIMU NA MENGINEYO.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.