ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 25, 2010

CHADEMA PEKEE YAJITANUA MIDAHALO MWANZA.

NI MDAHALO WA WAGOMBEA UBUNGE WILAYA YA ILEMELA ULIO FANYIKA LEO ASUBUHI KITRIMA HOTEL MWANZA CHA AJABU NI MGOMBEA MMOJA TU WA CHADEMA HAILE SAMSON NDIYE ALIYEJITOKEZA KTK MDAHALO HUO HIVYO KUPATA FURSA TOSHA YA CHAMA CHAKE KUULIZWA MASWALI NA KUZINADI SERA KWA MAPANA KATIKA MDAHALO WA SAA MBILI.

MGOMBEA HUYO SAMBAMBA NA KUTOA AHADI YA OFISI KWA WALEMAVU WILAYA YA ILEMELA NA KUSAIDIA UPATIKANAJI WA MADAWA YA NGOZI KWA NDUGU ZETU WALEMAVU WA NGOZI BW. HAILE SAMSON KWA KUSAIDIANA NA WANANCHI WAKE AMEAHIDI KUJENGA HOSPITALI YA WILAYA YA ILEMELA.

ALIPOPEWA FURSA YA KUJINADI NA KUOMBA KURA MGOMBEA HUYO WA UBUNGE ILEMELA ALISEMA "VYAMA VINAPITA LAKINI TANZANIA INABAKI PALEPALE, TUSICHAGUE VYAMA TUCHAGUE MTU. HATUNA TATIZO LA RASLIMALI, TATIZO TULILONALO NI VIONGOZI KUKIUKA MAADILI NA KUWA NA VIONGOZI MAFISADI" "MIAKA INAENDA MIAKA INARUDI MATATIZO YAKO PALE PALE, NA KILA KUKICHA NDIYO HAYO HAYO YANAYOZUNGUMZWA IWE NI MAJI, MIUNDO MBINU, MIGOGORO YA ARDHI, YOTE HAYA HAYAHITAJI DIPLOMA WALA DEGREE KUYATATUA, NI UMAKINI, UTASHI NA DHAMIRA THABITI YA KIUONGOZI"

JIMBO LA KIRUMBA LINA SIFA YA KUTOA WASUKUMA KANDANDA WAZURI MIAKA YA ZAMANI NA MIAKA YA SASA, VIWANJA NI MOJA YA NYENZO ZA KUKUZA VIPAJI, KERO INAKUJA MOJA YA VIWANJA MUHIMU KWA MAENDELEO YA SOKA WILAYA HIYO (FURAHISHA) KIMEMEGWA NA KUTUMIKA DAMPO LA TAKA.
MALALAMIKO YAMEFIKA IDARA ZOTE KULALAMIKIA KUHUSU HAKI YA MICHEZO NA SUALA ZIMA LA AFYA AKIWA KAMA MGOMBEA UNAAHIDI KUSURU VIPI WANANCHI WA JIMBO LAKO. KWA SWALI HILI NASIKITIKA NAFASI HAIKUPATIKANA TU! NAO MUDA 'ULIFUPIKA'!

TIMEKEEPER MWENDESHA MDAHALO MKURUGENZI WA MPC MWANZA BW. KASIAN AKIFUNGA MDAHALO KWA KUTOA SHUKURANI KWA USHIRIKIANO.

JAPO KWA CHATI NA WAANDISHI WA HABARI.

MDAHALO ULINOGA HADI WAKATI MGOMBEA HUYO AKITOKA ENEO LA UKUMBI WA MDAHALO NAO MUDA HAUKUTOSHA MASWALI YALIKITA PANDE ZOTE, MISINGI YA UONGOZI, ELIMU, AFYA, MICHEZO, WALEMAVU, HAKI ZA MTOTO NA MAMA, AJIRA, MIGOGORO YA ARDHI (KIWANJA KIMOJA KUMILIKIWA NA WATU WATATU) NAKADHALIKA. JIMBO LA ILEMELA LINA WAGOMBEA WATATU AMBAO NI BW. ANTHONY DIALO (CCM), BW. HAILE SAMSON (CHADEMA) NA BW. (CUF).

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.