ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 27, 2010

HOFU YA AJALI FEKI YALIKUMBA JIJI LA MWANZA . WANANCHI WAHAHA KUSAKA NDUGU ZAO WASAFIRI.

MARA BAADA YA TAARIFA ZA KUANGUKA KWA NDEGE HALI TETE YA SINTOFAHAMU PAMOJA NA HOFU VIMELIKUMBA LEO JIJI LA MWANZA. TAARIFA HIZO ZILIZO CHAGIZWA NA PILIKA PILIKA ZA MAGARI YA WAGONJWA KUTOKA ENEO LA TUKIO ZILIMEUSHITUA MJI NA VITONGOJI VYAKE HALI ILIYOSABABISHA UWANJA WA NDEGE WA MWANZA KUJAA WANANCHI KUTAZAMA EITHER NDUGU ZAO AU PENGINE KUPATA TAARIFA IKIWA NI PAMOJA NA KUJUA NINI CHANZO CHA AJALI.

ILINIBIDI KUSITISHA SHUGHULI NILIYOKUWA NIKIIFANYA MARA BAADA YA KUPATA TAARIFA ZISIZO NA MWELEKEO, WATU WAKIDAI NDEGE IMEANGUKA AIR PORT WAKATI IKITUA, WENGINE WAKIDAI KWAMBA KAMBI YA JESHI ILIYOPO KARIBU NA VIWANJA HIVYO IMEUNGUA, WENGINE WAKIDAI KUWA NDEGE ILIYOKUWA IKIRUKA KUTOKA MWANZA IMEANGUKA MUDA MCHACHE WAKATI IKIONDOKA ALIMURADI KILA MMOJA ALIKUWA NA LAKE (SI UNAJUA TENA WABONGO KWA UWONGO!?)

NAMI KAMA MWANDISHI MWAKILISHI NIKATIMKA MOJA KWA MOJA HADI AIR PORT KWENDA KUCHUKUWA NYUZI.

IKIWA NA NA MWENDO KASI WA KAZI AMBULANCE HII IKIWA NA MIILI YA WATU WALIOIGIZA MAJERUHI, NILIKUTANA NAYO ENEO LA GHANA ILEMELA MWANZA.

MENEJA WA UWANJA WA MWANZA ESTER B. MADALE AKATOA TAARIFA KWAMBA NDEGE YA ABIRIA YENYE USAJILI NAMBA SH-INT INAYOMILIKIWA NA SHIRIKA LA NDEGE LA INTERIOR AIR ILIYOKUWA NA ABIRIA 51 IKITOKEA KIGOMA KUJA MWANZA MAJIRA YA SAA 4:59 IMENGUKA WAKATI IKITUA NA KUUWA WATU 25.

MAJERUHI WENYE HALI MBAYA 15 NA ABIRIA WALIONUSURIKA WENYE HALI YA AFADHALI 11, MENEJA HUYO WA UWANJA AKATAJA KUWA UCHUNGUZI WA AWALI ULIONYESHA KUWA NDEGE HIYO ILIKUWA NA MAFUTA YA KUTOSHA KUMUDU SAFARI YA MASAA MANNE NA HATIMAYE SABABU ZA NDEGE KUANGUKA KWA NDEGE HIYO ZIKATAJWA KUWA NI HITILAFU UPANDE WA INJINI.

MARA BAADA YA KUKAMILIKA KWA TAARIFA YAKE NDIPO MENEJA HUYO WA UWANJA AKATUPA PICTURE HALISI KWAMBA TUKIO HILO LA AJALI HALIKUWA AJALI BALI ILIKUWA NI SEHEMU YA MAZOEZI YA JESHI LA ANGA AIR PORT MWANZA KUPIMWA NI JINSI GANI MAMLAKA HIYO UPANDE WA MWANZA ILIVYOJIPANGA KATIKA UOKOAJI IWAPO AJALI YA NDEGE IKITOKEA NA ZOEZI LIMEKUJA MARA BAADA YA KUTUNUKIWA CHETI CHENYE HADHI YA JUU CHA USALAMA WA ANGA NGAZI YA KIMATAIFA.

PICHANI WAANDISHI WA HABARI. 'WAJANJA WA MUJINI WAINGIZWA MUJINI' TEHE TEHE!! LENGO LA ZOEZI HILO NI KUTAKA KUONA USHIRIKIANO ULIVYO KUTOKA IDARA MBALIMBALI KAMA JESHI LA POLISI, HOSPITALI, UONGOZI WAWILAYA, MKOA NA IDARA MBALIMBALI ZA SERIKALI. KATIKA MKOA WA MWANZA ZOEZI KAMA ILI MARA YA MWISHO LILIFANYIKA MWAKA 2008.

HALI ILIKUWA MBAYA ZAIDI KWA NDUGU WA RUBANI WA NDEGE HIYO HEZRON GOLDEN AMBAYE ALIPATA USUMBUFU KUTOKA KWA MARAFIKI, NDUGU, MAJIRANI NA JAMAA ZAKE WOTE WANAOMFAHAMU NA HATA WAKATI NIKITOKA VIWANJANI HAPO RUBANI HUYO ALIKUWA AKIPOKEA SIMU KWA WATU WANAOMFAHAMU KUJUA HALI YAKE. BAADAE MAMBO YALIKWENDA SAFI...KUMBE ILIKUWA MAZOEZI!

Tupe maoni yako

1 comments:

  1. "HOFU YALIKUMBA YA AJALI FEKI YALIKUMBA JIJI LA MWANZA . WANANCHI WAHAHA KUSAKA NDUGU ZAO WASAFIRI."

    Heading ya hii habari imekaaje mkuu?

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.