CHANZO BIN ZUBEIR
Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
SIMBA
SC imepunguzwa kasi baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Mbeya City
katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Kwa
matokeo hayo, Simba inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 55,
baada ya kucheza mechi 24, wakifuatiwa na mabingwa watetezi, Yanga wenye
pointi 52 za mechi 23 ambao kesho watacheza ugenini dhidi ya Mtibwa
Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Mbeya City wao baada ya sare leo, wanafikisha pointi 30 baada ya kucheza mechi 24.
Katika
mchezo huo uliochezeshwa na refa Jacob Adongo wa Mara, hadi mapumziko
Mbeya City walikuwa tayari mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na Ditram
Nchimbi dakika ya 37 kwa shuti akimalizia kazi nzuri ya Raphael Daudi.
Shiza Kichuya ameifungia Simba bao la kusawazisha kwa penalti dakika ya 86
Pamoja na kutoka uwanjani ikiwa nyuma kwa bao 1-0, lakini Simba SC ndiyo waliotawala zaidi mchezo huo na kupoteza nafasi kadhaa nzuri za kufunga.
Pamoja na kutoka uwanjani ikiwa nyuma kwa bao 1-0, lakini Simba SC ndiyo waliotawala zaidi mchezo huo na kupoteza nafasi kadhaa nzuri za kufunga.
Beki
wa kulia, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ alipiga shuti kali dakika ya
24, lakini kipa Mmalawi wa MCC, Owen Chaima akadaka na Nahodha Jonas
Mkude naye alikaribia kuifungia Simba dakika ya 28 kama si shuti lake
kwenda nje baada ya pasi ya winga Shiza Kichuya.
Mshambuliaji
tegemeo wa timu hiyo, Mrundi Laudit Mavugo alikaribia kufunga dakika ya
32 kama si beki wa Mbeya City, Rajab Zahir kuokoa.
Kiungo
Muzamil Yassin alipiga shuti zuri baada ya krosi ya Hamadi Juma dakika
34, lakini mpira ukapaa juu na dakika ya 40 mshambuliaji mwingine
tegemeo wa Simba, Ibrahim Hajib nusura aipatie bao timu yake kama si
shuti lake kudakwa na Chaima.
Zaidi
ya bao lao, shambulizi lingine la maana Mbeya City walifanya dakika ya
25, Ditram Nchimbi akipiga shuti kali baada ya pasi ya Bryson Raphael,
lakini mpira ukaenda nje.
Hajib
aliisawazishia Simba SC kwa shuti la mpira wa adhabu dakika ya 65,
uliopigwa nje kidogo ya boksi la Mbeya Ciry baada ya Bryson Raphael
kuunawa mpira.
Baada
ya bao hilo, Mbeya City wakafunguka na kuanza tena kusaka ushindi
Uwanja wa ugenini na haikuwa ajabu walipofanikiwa kupata bao la pili
dakika ya 79, mfungaji Nahodha wake, Kenny Ally.
Hata
hivyo, Simba SC wakafanikiwa kusawazisha kupitia kwa Shiza Kichuya
aliyefunga kwa penalti dakika ya 86 baada ya Tumba Lui kumuangusha beki
Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kwenye boksi.
Kikosi
cha Simba SC kilikuwa: Daniel Agyei, Hamadi Juma, Mohammed Hussein
‘Tshabalala’, James Kotei, Abdi Banda, Jonas Mkude, Ibrahim Hajib/Mwinyi
Kazimoto dk80, Muzamil Yassin/Mohammed ‘Mo’ Ibrahim dk54, Laudit
Mavugo, Said Ndemla na Shiza Kichuya.
Mbeya
City: Owen Chaima, Haruna Shamte, Majaliwa Shaaban, Tumba Lui, Rajab
Zahir, Sankhani Mkandawile/John kabanda, Raphael Daudi, Kenny Ally,
Ditram Nchimbi, Mrisho Ngassa/Ayoub Semtawa dk69 na Bryson Raphael/Zahor
Pazi dk90.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.