Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema yeye ni sawa na mashine ya kusaga na kukoboa ambayo ukiweka miguu unageuka sembe.
Gwajima amesema hayo leo asubuhi katika ibada inayoendelea kanisani kwake hivi sasa akieleza kuwa, "Baba wa familia amechokozwa kuwa anavuta unga watoto wamechachamaa wanataka baba ampige adui yake, nitaendelea kupiga bila kuogopa chochote."
"Watu wananiambia niache kumpiga mbona hawakumwambia yeye aache kunipiga, nitampiga tu na bado kazi inaendelea."
"Yeye alisema awamu ya kwanza, akaja na awamu ya pili, akaja na awamu ya tatu, mimi nimerusha kombora awamu ya kwanza tu, sijaja awamu ya pili na awamu ya tatu unalilia nini?"
"Mimi nimerusha awamu ya kwanza, tena kakipande tu, kakipande kale nimekarusha kamejaa ahadi, ndani yake kulikuwa na ahadi ya mambo kadha wa kadha wa kadha wa kadha ni ka-kipande tu"
"Sikiliza nikwambie msumeno ukienda mbele unakata, ukirudi nyuma unakata"
Sasa watu wanasema Gwajima imetosha, Gwajima nini na nini, Gwajima umemaliza.....Sikiliza vizuri, nilisema wiki iliyopita mimi nataka neno moja tu... Nataka hiviiii ..... SAMAHANI KWA MAANA NALIISALITI DAMU ISIYO NA HATIA, Ukisema hivyo Upendo unarudi mahala pake" Alisema Gwajima.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.