Mkuu wa Mkoa wa GeitaMeja Jenerali Mstaafu,Ezekiel Kyunga akiteketeza dhana haramu ambazo zimekamatwa katika oparation iliyofanyika kwenye mialo iliyopo Mkoani Geita lengo likiwa ni kutokomeza uvuvi haramu ambao umeendelea kwa kasi kwenye mialo ya Izumacheli na Mganza. |
Baadhi ya wananchi wakivuta kokolo wakipeleka eneo la kuchomea. |
Dhana haramu za uvuvi zikiwa zimekusanywa kwaajili ya kuchomwa kwenye mwalo wa dala dala uliopo kijiji cha Nyasalala kata ya Bukondo. |
Meza kuu ikongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita ,wakisiliza kwa makini taarifa ambayo ilikuwa ikisomwa na afisa uvuvi. |
Afisa
mfawidhi udhibiti ubora wa samaki na usimamizi wa rasilima za uvuvi
kanda ya Mkoa wa Geita Shafii Ramadhan Kiteri,akitoa taarifa ya zoezi
la oparesheni Tokomeza uvuvi haramu. |
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Geita,Bi Janneth Mobe akimkaribisha Mkuu wa Mkoa kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Nyasalala. |
Mkuu wa Mkoa wa GeitaMeja Jenerali Mstaafu,Ezekiel Kyunga,akizungumza na wananchi wa kijiji cha nyasalala juu ya wao kutoa ushirikiano kwa serikali katika kupambana na uvuvi haramu. |
Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Geita wakati alipokuwa akizungumza. |
Zoezi la uchomaji wa dhana hizo za uvuvi likiendelea. |
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE BLOG
WITO umetolewa kwa wananchi ambao wanafanya shughuli za uvuvi Mkoani
Geita,kuendelea kutoa ushirikiano kwa serikali kwa kuwafichua wale ambao
wamekuwa wakijihusisha na shughuli ya uvuvi haramu katika mialo iliyopo
Mkoani Humo.
Rai
hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja Jenerali mstaafu Ezekiel
Kyunga wakati wa zoezi la kuteketeza zana haramu za uvuvi kwenye
Mwalo wa daladala uliopo kijiji cha Nyasalala kata ya Bukondo
zilizokusanywa ndani ya miezi miwili kuanzia Januari hadi Februari mwaka
huu.
Aidha
mh Kyunga amesema kuwa uhifadhi wa rasilimali zilizopo kwenye ziwa
viktoria ni muhimu kwa kila mwananchi kwani endapo uvuvi haramu
ukiachiwa madhara yake yanaweza kuwa ni makubwa kwa viumbe ambavyo vipo
katika ziwa.
“Ndugu
wananchi kwa kweli uhifadhi rasilimali zilizomo katika ziwa letu hili
ni muhimu ,ni muhimu kwa sasa na vile vile kwa baadae isipokuwa mimi
nisisitize sisi wote hapa kwa ajili ya ustawi wetu na vizazi vijavyo
tuone kwamba tuna wajibu wa kuhifadhi mazingira na matumizi bora ya ziwa
letu hili,tukilivuruga kama hawa wenzetu wanavyolifuruga kwa kuendesha
uvuvi haramu na uharibifu wa mazingira hasara ambayo wanatuachini ni
kubwa sana hawa watu kwa lugha nyingine naweza kusema ni wachawi”Alisema
Kyunga
Hata
hivyo katibu wa BMU mwalo wa Daladala,Methusela Samweli amemweleza
Mkuu wa Mkoa kuwa changamoto kubwa ambayo wanapambana nazo katika zoezi
la kutokomeza uvuvi haramu ni kukosekana kwa vitendea kazi ikiwemo
kukosekana kwa Boti kutokuwepo kwa ulinzi wa kutosha ambao utasaidia
usalama wakati wa doria.
Karoli
Makoba na Baraka Mkwazu ni wananchi ambao wapo kwenye mwalo huo
wameiomba serikali na BMU kuweka uhusiano wa karibu kwa kushirikiano
hili kutokomeza tatizo la uvuvi haramu ambalo limeendelea kushamiri kwa
kasi kubwa hususani kwenye mialo ya Izumacheli na Mganza.
Kwa
mujibu wa maelezo ya afisa mfawidhi udhibiti ubora wa samaki na
usimamizi wa rasilima za uvuvi kanda ya Mkoa wa Geita Shafii Ramadhan
Kiteri,ameelezea kuwa Doria ambayo imefanyika kwa miezi miwili
imefanikisha kukamata jumla ya samaki wachanga ambao Kg 7,682,Mitumbwi
19,watuhumiwa 12,gari moja Hiace na Gari ya pili aina ya Fuso
Tandam,pikipiki 3,Nyavu za makila 1,261,Makokoro ya kuvutwa nchi kavu
23,Dududu 41na Timba 17.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.