ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 3, 2017

WAANDISHI WA HABARI KANDA YA ZIWA WAKOMAZWA KUKABILIANA NA SHERIA MPYA YA HUDUMA ZA HABARI

Mmoja wa wakufunzi wa mafunzo kwa wanahabari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Mwanza, Mara, Geita na Simiyu, Marie Engel, akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa kuandika habari juu ya Haki za Binadamu upande wa afya.

MAFUNZO hayo ya siku mbili tangu jana, yameandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) Tawi la Tanzania, yakilenga kuwajengea wanahabari uelewa juu ya Sheria Mpya ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 na Kanuni zake za mwaka 2017 ili kuwasaidia katika utendaji wa majukumu yao bila kukinzana na sheria na kanuni hizo.

Pamoja na mambo mengine, washiriki wa mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Taasisi ya Friedrick Ebert Stiftung (FES) Tanzania, wamefundishwa sheria na taratibu za kuandika na kuripoti habari/ makala kuhusu haki za binadamu kwa kuangazia sekta ya afya juu ya habari na makala za magonjwa ya kuambukiza kama HIV/Ukimwi ambapo wameahidi kuifikisha elimu hiyo kwa wenzao na pia kuitumia vyema katika kuboresha utendaji kazi

Wakili James Marenga akifunguka mbele ya kipaza sauti cha Jembe Fm kipindi cha Kazi na Ngoma. BOFYA PLAY KUSIKIA

Hii inaitwa noa bongo, ilikuwa ni zamu ya mwandishi wa ITV Victor Bariet akirushiwa mpira na hapa akifunguka alichojifunza kwenye mafunzo hayo.

Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo.

Hii inaitwa noa bongo, ukirushiwa mpira unaeleza ulichojifunza kwenye mafunzo hayo.

Mmoja wa wakufunzi wa mafunzo kwa wanahabari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Mwanza, Mara, Geita na Simiyu, Marie Engel, akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa kuandika habari juu ya Haki za Binadamu upande wa afya.

Mmoja wa wakufunzi wa mafunzo kwa wanahabari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Mwanza, Mara, Geita na Simiyu, Marie Engel, akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa kuandika habari juu ya Haki za Binadamu upande wa afya.

Mmoja wa wakufunzi wa mafunzo hayo, Wakili James Marenga, akitoa somo.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo. Wakimsikiliza Afisa Habari na Utafiti kutoka Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Gasirigwa Sengiyumva, hayupo ichani.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo kwa umakiiini zaidi.

Mwakilishi wa Metro Fm Mwanza, Alphonce Kapela, akichangia mada kwenye mafunzo hayo.

Picha ya pamoja, waandaaji wa mafunzo, wakufunzi wa mafunzo pamoja na washiriki wa mafunzo ambao ni wanahabari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Mwanza, Mara, Geita na Simiyu.

Picha ya pamoja, waandaaji wa mafunzo, wakufunzi wa mafunzo pamoja na washiriki wa mafunzo ambao ni wanahabari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Mwanza, Mara, Geita na Simiyu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.