ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, December 2, 2022

DKT. NDUMBARO ATAKA MRADI WA KITUO JUMUISHI CHA TAASISI YA KISHERIA MWANZA KUZINGATIA MATUMIZI SAHIHI YA FEDHA.

 NA ALBERT G.SENGO/ MWANZA

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt, Damas Ndumbaro ametaka mradi wa kituo jumuishi cha taasisi ya sheria kinachojengwa Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza kuzingatia matumizi sahihi ya fedha yenye tija na maslahi Kwa Nchi.

Hayo ameyabainisha wakati wa uwekaji wa jiwe la Msingi na kueleza kuwa ujenzi wa jengo hilo linapaswa kuwa kichocheo Kwa ujenzi wa majengo mengine Kama hayo katika sehemu nyingine za Nchi. Dkt, Ndumbaro ameeleza kuwa ili kuweza kufikia malengo ni lazima wahakikishe wanatembea katika dira na dhima ya wizara na kuendelea kuimarisha miundmbinu katika kuhakikisha uapatikanaji wa haki unakuwa kiurahisi Kwa Kila mtu. "Kutokana na hili nipende kutoa shukrani Kwa serikali ya awamu ya sita imeendelea kutoa fedha Kwa mahakama ambapo miradi mbalimbali imeendelea kujengwa ikiwemo ujenzi wa vituo jumuishi katika Mikoa mbalimbali" Alisema Ndubaro. Aidha ametoa wito Kwa mkandarasi wa mradi huo kuhakikisha anakamilisha Kwa wakati jengo Hilo na Kwa ubora kwani fedha zinazotumika ni za wananchi. Naye Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk Eliezer Feleshi ameeleza kuwa ujenzi wa vituo jumuishi utasaidia kuwezesha taasisi za kisheria za serikali, Wizara pamoja na wadau muhimu Kwa pamoja kuongeza tija katika kutoa huduma. Feleshi amesema kuwa mpango huo utafanikisha kazi zinazofanywa na mahakama mtandaoni pamoja na kuondoa zinazowakabili katika maeneo yenye mahakimu wengi kuliko mawakili wa serikali. Akitoa taarifa ya ujenzi wa kituo hicho Mkurugenzi wa Huduma za Ushauri kutoka Wakala Majengo Tanzania (TBA), Wencelaus Kizaba amesema jengo hilo litagharimu zaidi ya Sh Bil, 3,181,548,096.83 hadi kukamilika kwa ujenzi huo. Kizaba amesema kuwa ujenzi wa jengo hili ulianza aprili 26 mwaka huu na unatarajia kukamilika oktoba 25 mwaka 2023 kwani mpaka hivi sasa upo asilimia 35 ya ujenzi wa kazi zote za mkataba. Ameeleza kuwa mradi huo umetoa ajira mbalimbali kwa wataalamu na wafanyabiashara wadogo wadogo ,umetoa mafunzo kwa wanafunzi wa vyuo vya nchini "Vifaa vinavyotumika kwenye ujenzi huu vinatoka kwenye viwanda vyetu vya ndani ikiwemo Saruji,Rangi,Mabomba na baadhi vitatoka kwenye viwanda vya nje,"amesema Kizaba. Kwa upande wake mwakilishi wa Mbunge wa jimbo la Nyamagana,Florah Magabe ameipongeza Serikali kwa kuanzisha vituo jumuishi vitakavyosaidia kukabiliana na vishoka.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.