Na Victor Masangu,Pwani
Imeelezwa baadhi ya watoto wenye ulemavu wa viungo katika mkoa wa Pwani bado wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa kutokuwa na mahitaji yao muhimu na kupelekea kuishi katika mazingira ambayo sio rafiki kwao.
Katika kuliona hilo Kikundi cha Pwani generation Qeen kimeamua kutumia fafrija ya utoaji wa tuzo kwa mwanamke sahihi fete kurudisha matendo ya huruma kwa kutoa msaada wa baiskeli zipatazo 15 kwa watoto wenye ulemavu pamoja na magongo ya kutembelea.
Kikundi hicho Cha Pwani generation Qeens 'Mwanamke wa shoka' kwa sasa kimetimiza miaka minne tangu kuanzishwa kwake na kimekuwa kikisaidia na kutoa michango mbali mbali kwa jamii pamoja na wenye mahitaji maalumu.
Akizungumza katika tafrija za mwanamke sahihi fete zilizofanyika Wilayani Kibaha,Mwenyekiti wa Kikundi hicho Betty Msimbe alisema kwamba kwa mwaka huu wameweza kuboresha zaidi tuzo hizo ambazo zimeenda sambamba na kutoa msada wa baiskeli hizo 15 zenye thamani ya Shilingi zaidi ya milioni 6.
"Mwaka huu tumefanya maboresho katika tuzo zetu mbali mbali maana licha ya kutoa tuzo hizo kwa wanawake na wanaume tukaona kuna umuhimu wa kuisadia jamii hasa kwa watu wenye ulemavu kwani katika Mkoa wa Pwani wapo wengi,"alisema Msimbe.
Aidha Mwenyekiti huyo alibainisha kwamba wao Kama Kikundi wamejiwekea yao katika siku za usoni kuwafikia watoto 100 ambao watawapatia msaada wa vifaa mbali mbali ikiwemo kuwapa baiskeli ambazo zitawasaidia hata kwenda shule kwa urahisi.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa katika tafrija hiyo ambayo imehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na vikundi ambavyo vimeweza kupatiwa vyeti vya pongezi pamoja na tuzo Bora kutokana na kazi zao pamoja na ushiriki wao katika shughuli za kijamii.
Katika hatua nyingine alimpongeza Rais wa awamu ya sita Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuwatumikia wananchi na kuwaletea chachu ya maendeleo ikiwa sambamba na kutenga fedha ambazo zimeweza kusaidia katika shughuli za kijamii.
Kwa upande wake afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Pwani Recho Chacha ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tafrija hiyo amekipongeza kikundi hicho kwa kuweza kuandaa tuzo hizo pamoja na kutoa msaada wa baiskeli 15 kwa watoto wenye ulemavu.
"Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza kwa dhati kikundi hiki cha Pwani generation Qeens kwa kuisaidia jamii kwa kutoa msaada wa baiskeli kwa watoto walemavu ikiwa sambamba na kutoa tuzo kwa wanawake na wanaume ambao wamefanya vizuri katika kazi zao,"alisema.
Aidha aliwaasa wazazi kuhakikisha wanakuwa karibu na watoto wao na kuwapa malezi na maadili bora ambayo yataweza kuwasaidia kuepukana na mambo ambayo hayafai kufanywa katika jamii.
Pia aliitaja jamii kuachana kabisa na tabia ya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto wao na badala wake wahakikishe wanazuia na kupinga kabisa vitendo hivyo kwani ni kinyume kabisa na sheria na taratibu za nchi.
Nao baadhi ya watoto hao walemavu ambao wamepatiwa msada wa baiskeli hizo wamekishukuru Kikundi hicho Cha Pwani generation Qeen kwa kufanya matendo ya huruma kwani kwa upande wao msada huo utakuwa ni mkombozi mkubwa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.