ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, December 2, 2022

MWILI WA ASKOFU KWANGU WAOKOTWA UKIELEA ZIWA VICTORIA.

NA ALBERT G. SENGO/ MWANZA Askofu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Victoria Nyanza (DVN), Boniphace Kwangu (61) amekutwa amefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema kuwa, marehemu aliaga familia yake na kuelekea wilaya ya Sengerema kwa ajili ya kupokea malipo ya mwisho ya shilingi 2,500,000/= baada ya kuwa ameuza eneo lake pamoja na nyumba kwa kanisa la KKKT- Sengerema. Hata hivyo hakuweza kulipwa kiasi hicho cha fedha kwa kuwa wanunuzi walimtaka awasilishe nyaraka ya umiliki wa eneo hilo hivyo, alirudi Mwanza mjini kwa ajili ya kushughulikia nyaraka hizo. Ilipofika jioni ya siku hiyo familia yake walipata wasiwasi kuhusu alipo Boniphace William Kwangu kwani hakuwa amerudi nyumbani pia alikuwa hapatikani kwenye simu yake ya mkononi. Kutokana na hali hiyo ilibidi familia yake watoe taarifa Kituo cha Polisi Kirumba. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na familia na watu mbalimbali lilianza kufanya ufuatiliaji ili kubaini alipo askofu. ZAIDI VIDEO


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.