ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 3, 2022

WAKULIMA IRINGA WANUFAIKA NA MRADI WA USAID LISHE ENDELEVU.

 

Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Mhandisi Leonard Masanja akiongea wakati wa kikako kazi juu ya kupunguza udumavu mkoa wa Iringa kupitia Mradi wa USAID Lishe Endelevu
Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Mhandisi Leonard Masanja akiongea wakati wa kikako kazi juu ya kupunguza udumavu mkoa wa Iringa kupitia Mradi wa USAID Lishe Endelevu
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakiwa makini kuwasikiliza viongozi
Nengilangen't Kivuyo-Meneja Mradi wa USAID Lishe Endelevu Mkoa wa Iringa
akiwa kwenye moja la shamba la mfano.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

MRADI wa USAID Lishe Endelevu umeanzisha mashamba ya mfano 186 na kuwafikia na kuwajengea uwezo wakulima 6,842 ikiwa ni sehemu ya mikakati yake ya kuusaidia Mkoa wa Iringa kukabiliana na udumavu.

Takwimu za mwaka 2018 zinaonesha katika kila watoto 100 wenye miaka chini ya mitano mkoani humo, 47 sawa na asilimia 47 wamedumaa kutokana na lishe duni.

Mratibu wa USAID Lishe Endelevu (Kilimo Mifugo na Uvuvi), Samwel Kitila alisema hatua hiyo imelenga kuiwezesha jamii kuongeza uzalishaji na ulaji wa vyakula vyenye virutubishi vingi.

Aliongeza kwa kusema kuwa Mradi wa USAID Lishe Endelevu kwa kushirikiana na Serikali ulianzisha Mabwawa 12 ya samaki (12000Vifaranga vya samaki) 2021 lakini hivi tunavyoongea mkoa wa Iringa una mabwawa 52 ya samaki(31840).

Kwa upande mazao Lishe (Mahindi Lishe,Maharage Lishe na Viazi) mwamko kwa wakulima umekuwa mkubwa sana mfano kuna kata inaitwa Nyanzwa-Kilolo

 Mradi wa Lishe Endelevu ulitoa mbegu za kutosha eneo la robo ekari 2020 lakini mpaka kuna zaidi ya Ekari 17 ambazo zinalimwa Viazi Lishe ambavyo ni kwa ajili ya kuboresha hali ya Lishe lakini pia kama chanzo mbadala cha kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja.

Ukilinganisha na awali  ulaji wa mazao mchanganyiko na mazao mchanganyiko umeongezeka sana kwenye maeneo yote ya utekeleza wa Mradi.

Alisema mradi haukuishia kwa wakulima kwani ulifanya pia kazi ya kuvijengea uwezo Vikundi 99 vya kuweka na Kukopa(VSLA) ili viwe na sifa ya kupesheka na tayari 50 kati yake vimefanikiwa kupata mkopo wa Sh Milioni 83 ili kuendelea kukuza shughuli zao za kijasiriamali.

“Mradi pia umedhamiria kuongeza upatikanaji na utoaji wa huduma bora za lishe katika ngazi ya vituo vya afya na jamii kwa kuimarisha uwezo wa watoa huduma za afya,” alisema.

Katika kikao cha pamoja cha wadau kilicholenga kujua mafanikio ya utekelezaji wa mradi huo, changamoto na utatuzi wake ili kuweka mikakati endelevu,

Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Mhandisi Leonard Masanja aliwataka viongozi na watendaji wa mkoa kushirikiana na wadau ili kupunguza udumavu mkoani humo.

Mhandisi Masanja alisema;“Kila mmoja wetu anatakiwa kuhakikisha anatoa huduma bora za lishe na kuwafikia walengwa wote ili kupunguza athari za utapiamlo na hasa udumavu miongoni mwa jamii yetu.”

Kwa kupitia msaada wa Watu wa Marekani, Masanja alisema mkoa wa Iringa unatambua mchango mkubwa wa Mradi wa USAID Lishe Endelevu wa mwaka 2018 hadi 2023 katika kutatua tatizo la lishe duni, utapiamlo.

Alisema mradi huo umechangia katika maeneo mengi yakiwemo; kuongeza hamasa ya mabadiliko ya tabia kwa wanawake wajawazito, wanaonyonyesha, watoto walio chini ya miaka mitano na vijana wa rika balehe kwa kupitia wanawake vinara, vikundi malezi na klabu za lishe. 

Eng. Masanja aliwataka viongozi na watendaji wa Mkoa wa Iringa wameshauriwa kushirikiana katika kuhakikisha udumavu unapungua ili kuwa na watoto wenye afya ya mwili na akili. 

Alisema kuwa lishe ndiyo msingi wa maisha ya mwanadamu na kuongeza kuwa afya ya mwanadamu ikiharikiwa kwa lishe duni katika siku elfu moja (1,000)za mwanzo wa uhai, haziwezi kurekebishika kwamwe katika maisha yote ya mwanadamu.

Eng. Masanja alisema kila mmoja wetu anatakiwa kuhakikisha kuwa anatoa huduma bora za lishe na kuwafikia walengwa wote ili kupunguza athari za utapiamlo hasa udumavu

Pia aliwasihi viongozi kusimamia zoezi la mipango na bajeti za lishe kwa mwaka 2023/24 kuanzia ngazi ya kijiji hadi halmashauri ili kuhakikisha shughuli ambazo zimepangwa  zinaendelea  kutatua changamoto zilizopo katika jamii.

 

“Vituo vyote vya kutolea huduma za afya,shule na serikali mtambuka zipange shughuli za lishe zitakazosaidia kupunguza utapiamlo,”alisema Masanja.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mradi wa USAID Lishe Endelevu Tanzania Dk Joyceline Kaganda, Dk Benny Ngereza alisema mbali na Iringa, mradi huo wa miaka mitano unatekelezwa katika mikoa ya Rukwa, Morogoro na Dodoma.

 Dkt. Joyceline Kaganda, alisema kuwa lengo kubwa ya kikao hicho ni kufanya tathimini ya utekelezaji wa mradi kwa miaka minne, hasa katika mkoa wa Iringa.

Dkt. Ngereza aliwataka maofisa mipango, wahasibu na maofisa lishe wa halmashauri kusimamia upangaji na utekelezaji wa shughuli za lishe ili kupunguza changamoto za lishe duni.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.