ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 3, 2022

MBUNGANI FC WAKABIDHIWA MILIONI MOJA NA DC MOYO.

 

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akikabidhi kiasi cha shilingi milion moja kwa viongozi wa timu ya mbugani FC
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akipokea mipira kutoka kwa kampuni ya CRJE (EAST AFRICA) LTD kupitia kwa Meneja mradi Zhang linjie kwa ajili ya kuiwezesha timu hiyo kufanya mazoezi
Wachezaji na wadau wa soka wa kata ya Mboliboli wakiwa kwenye hali ya furaha 
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa sambamba na diwani wa kata ya Mboliboli na kaimu afisa tarafa ya Pawaga.


Na Fredy Mgunda,Iringa.

Timu ya Soka ya Mbugani Fc ya kata Mboliboli wilayani Iringa imekabidhidhiwa kitita Cha shilingi milioni milioni Moja iliyotolewa na wadau wa soka wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya kama sehemu ya pongezi baada ya kutwaa ubingwa katika mashindano ya Mbomipa Cup.

 

Kiasi hicho Cha Fedha kimetolewa kupitia harambee iliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo ambapo amewahimiza wadau wa soka Wilayani Iringa kuisaidia Timu hiyo Ili kuiwezesha kutatua Changamoto zinazoikabili ikiwemo ukosefu wa vifaa vya Michezo na fedha Kwa ajili ya uendeshaji wa Timu hiyo.

 

Moyo amesema Timu hiyo imeonesha ukomavu Kwa kutwaa ubingwa wa kombe la MBOMIPAkupitia Michezo iliyojikita katika kuhamasisha Utunzaji wa Mazingira na uhifadhi wa Wanyamapori katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuchochea Ulinzi wa Wanyamapori kwalengo la kuvutia watalii nchini

 

Katika Risala yake Kwa washiriki wa harambee hiyo wakiwemo wachezaji wa Timu ya Mbugani Fc Mkuu wa Wilaya Iringa Mohamed Moyo amewataka kuwa mabalozi wa uhifadhi Kwa kuwa mstari wa mbele kuwafichua wahalifu wanafanya ujangiri katika hifadhi Ili kuwezeshabhatua za kisheria kuchukuliwa.

 

Katika hafla hiyo kampuni ya CRJE (EAST AFRICA) LTD kupitia kwa Meneja mradi Zhang linjie ilichangua mipira miwili kwa ajili ya kuiwezesha timu hiyo kufanya mazoezi kwa ajili ya mashindano ya kiwilaya na mkoa.

 

katika halfa hiyo ya kuwapongeza mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alifanikisha kuchangisha kiasi cha shilingi milioni moja kwenye harambee waliyoifanya siku ya kuwapongeza.

 

Timu ya Soka ya Mbugani Fc ya kata Mboliboli wilayani Iringa inakabiriwa na changamoto ya ukosefu wa vifaa vya mazoezi kama vile jezi,bipsi,viatu vya wachezaji,vifaa vya golikipa,koni,nyavu na mipira hivyo wamewaomba wadau mbalimbali kuwachangia ili waweze kufikia malengo wanayoyakusudia.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.