ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, December 1, 2022

KYLIAN MBAPPE: YAIBUKA SABABU ZA STAR HUYO WA PSG KUKATAA KUCHEZA CAMEROON KWENYE KOMBE LA DUNIA

'FROM ZERO TO HERO' Kylian Mbappe  yuko katika kiwango kizuri akiwa na Ufaransa kwenye Kombe la Dunia, lakini angechezea Cameroon.

BABA yake mshambuliaji nyota wa Ufaransa Kylian Mbappe amesimulia yaliyojiri, na kumlazimu mwanawe kuwachezea wabingwa watetezi badala ya Cameroon. 


Mbappe alizaliwa mjini Paris na baba raia wa Cameroon Wilfried, na mama mzawa wa Algeria, lakini alifanya jitihada za kucheza soka la timu ya taifa hilo la Bara Afrika ya Kati ambako baba yake alizaliwa. 


Kutoka kushoto ni Mama wa Mbape, Mbape, Mdogo wake Mbape na Baba yake Mbape.

Mnamo 2018, Wilfried alidai kuwa mwanachama wa Shirikisho la Soka la Cameroon alimuitisha pesa kabla ya kumjumuisha mwanawe katika kikosi cha Indomitable Lions. 


 "Mwanzoni, nilitaka mwanangu achezee Cameroon lakini, mtu fulani katika Shirikisho la Soka la Cameroon alitoza kiasi cha pesa ambazo sikuwa nazo ili kumfanya acheze. 

Kutoka kushoto ni Mbape, Baba yake na Mdogo wake.


Wafaransa hawakutoza chochote." Mnamo 2018, Mbappe alikuwa katika kiwango cha kuvutia kwenye Kombe la Dunia nchini Urusi huku akifunga mabao manne, likiwemo moja katika ushindi wa 4-2 dhidi ya Croatia kwenye fainali. 


Aliweka historia ya kuwa kinda wa pili kufunga katika fainali ya Kombe la Dunia baada ya gwiji wa Brazil Pele. 


Ripoti za kuaminika zinaonyesha kuwa rushwa imekithiri katika timu za taifa za barani Afrika, ambapo ubora wa wachezaji hauzingatiwi. 


Ni nafasi ya kipekee kuchezea timu ya taifa, na Kylian anaamini kwamba wachezaji hawapaswi kulipwa ili kutumikia nchi yao. Kylian Mbappe aling'aa katika ushindi wa Ufaransa wa 2-1 dhidi ya Denmark katika mchezo wao wa pili wa Kundi D kwenye Kombe la Dunia la FIFA la 2022. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.