NA PETER FABIAN, BUCHOSA
Cheyo ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Bariadi Mashariki mkoani Simiyu, akimuelezea marehemu huyo, alifariki Aprili 30 mwaka huu katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza, alipokuwa akipatiwa matibabu na kuzikwa Mei 5 mwaka huu nyumbani kwake na mazishi hayo kuhudhuliwa na viongozi wa UDP na viongozi wa serikali, CCM na Mamia ya wananchi wa Kijiji cha Kakobe.
Awali akitoa salamu hizo za CCM kwa niaba ya Katibu Mkuu Kinana, Katibu wa CCM mkoani Mwanza, Miraji Mtaturu alisema CCM ilipokea kwa masikitika kifo cha mzee huyo aliyekuwa miongoni mwa wajumbe walioshirikiana na hayati Baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere, kutafuta Uhuru wa Tanzania akiwa mwasisi wa Chama cha TANU.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mbunge wa Jimbo la Buchosa Dk. Chrles Tizeba akitoa salam kwa waombolezaji na wafiwa, viongozi wa UDP na wananchi wa jimbo hilo, alisema marehemu alikuwa mzalendo wa kweli na mmoja wa wazee wake washauri, alimtia moyo katika shughuli za kisiasa na hakutaka kumuombea njaa adui yake.
Ibada ya mazishi ya Bogohe, iliongozwa na Mchunhaji Alphaxard Kabui wa AIC Kakobe, alisema mwili wa kufa na uharibikao utakapovaa kutokufa, neno lililoandikwa litatimia, mauti itamezwa kwa kushindwa kwani uchungu wa mauiti nidhambi na nguvu ya dhambi ni torati, watu wamshukuru Mungu, Yesu Kristo aliwapa nguvu ya kushinda dhambi, watashinda kila uovu wakimcha Mungu.
MWENYEKITI wa Chama cha UDP taifa, John Cheyo, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdullahman Kinana na Dk. Fotunatus Masha aliyewahi kuwa Makamu wa Mwenyekiti wa UDP taifa wamlilia na kutuma salamu za rambirambi mazishi ya mwasisi wa Chama cha TANU na Mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu ya Chama cha UDP taifa, marehemu Mzee Lameck Bogohe (93) , aliyezikwa juzi.
Marehemu Bogohe alizikwa juzi katika kijiji cha Kakobe Jimbo la Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza, katika wasifu wa marehemu Bogohe henzi ya uhai wake alikuwa mmoja wa wajumbe 17 walikuwa waasisi wa TANU mwaka 1954 kabla ya kuungana na Afro Shiraz Part mwaka 1977 na kuzaliwa CCM baadaye mwaka 1993 kuamua kujiunga na UDP.
Awali akitoa salamu hizo za CCM kwa niaba ya Katibu Mkuu Kinana, Katibu wa CCM mkoani Mwanza, Miraji Mtaturu alisema CCM ilipokea kwa masikitika kifo cha mzee huyo aliyekuwa miongoni mwa wajumbe walioshirikiana na hayati Baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere, kutafuta Uhuru wa Tanzania akiwa mwasisi wa Chama cha TANU.
“Katika mazishi haya namwakilisha Katibu Mkuu wa CCM taifa, Comred Kinana aliyenituma kwa niaba yake nimuwakilishe, nasema UDP mmetutendea haki kutualika kuja kumstili mzee wetu marehemu Bogohe, poleni wananchi wa Buchosa na wana UDP kuondokewa na mshauri na mpigania Amani,” alisema Mtaturu.
Huku akiongea na kuvuta hisia za waombolezaji na kuwafanya wampigie makofi (licha ya kuwa msibani) aliposema “Tuishi duniani kwa kutenda mema na kuhubiri amani kama marehemu alivyofanya akiwa hai, vyama vya siasa vipo tu wanachama wake ni watanzania, marehemu alianzia TANU, kafia UDP, siasa isiwe sababu ya kututenganisha, ituunganishe na tuvumiliane na kusisitiza amani na upendo,”alisisitiza.
Mtaturu alipongeza jitihada za marehemu kusimamia amani na umoja wa kitaifa wakati wa uhai wake, alieleza kuwa waasisi hao walitanguliza ‘Tanzania kwanza’ mtu na Chama akafuatia baadaye na kuhoji, amani ikikosekana kutokana na siasa za uchochezi na kusabisha mauaji, kukawa na vurugu watu wauane wanasiasa kura wataomba kwa nani ?.
Katibu huyo alipigiwa makofi alipodai, historia ya marehemu Bogohe ni kubwa katika taifa hili kwani alipigania amani hivyo kumuenzi kwa maneno haitoshi bali tuwakatae watu wanaovuka mipaka ya demokrasia na kuchochea uvunjifu wa amani ili taifa limwage damu.
“Nilipokea kwa masikitiko taarifa za msiba huu na haitoshi nimekuja kushiriki nanyi wananchi wenzangu, marehemu alikuwa mzalendo, hakuwa na usemi wa adui yako muombee njaa, alinipa ujasili katika changamoto za kisiasa kwa ushauri hivyo wana Buchosa tumeondokewa na hazina mhimu, tuienzi kwa vitendo,” alieleza Tizeba.
Ibada ya mazishi ya Bogohe, iliongozwa na Mchunhaji Alphaxard Kabui wa AIC Kakobe, alisema mwili wa kufa na uharibikao utakapovaa kutokufa, neno lililoandikwa litatimia, mauti itamezwa kwa kushindwa kwani uchungu wa mauiti nidhambi na nguvu ya dhambi ni torati, watu wamshukuru Mungu, Yesu Kristo aliwapa nguvu ya kushinda dhambi, watashinda kila uovu wakimcha Mungu.
Ndugu jamaa na marafiki msibani. |
Eneo walilokaa watoto wa marehemu. |
Mbunge wa Jimbo la Buchosa Dk. Chrles Tizeba akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Bogohe. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.