Nimetembelea Shule ya Msingi Buhangija mkoani Shinyanga ambayo hutunza watu wenye Ulemavu mbalimbali na kwa sasa imegeuzwa pia kuwa kituo cha watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino). Hapo shuleni nimekutana na Kabula Nkalango (14) mmoja wa wahanga wa mauaji ya Albino ambaye alinusulika kuuawa na wauaji kutoweka na mkono wake.Anaomba msaada wako kumuwezesha kupata mkono wa bandia au vifaa mbalimbali vya masomo. kama uko Tayari wasiliana nami nitakuunganisha na mkuu wa shule yake.
Fredrick Katulanda
Mwandishi wa habari
Mwananchi Communication
Mwanza.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment