Uzindizi wa kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika kwa mkoa wa Mwanza umefanyika rasmi leo kwenye Uwanja wa KWIDECO katika Tarafa ya Ngudu Wilayani Kwimba ambapo masuala ya ukosefu wa maji, uhaba wa chakula, ukame, ulinzi na usalama ndiyo yalikuwa yameteka sehemu ya mkutano huo wa uzinduzi ambapo kilele chake kitakuwa tarehe 9Desemba mwaka huu.
Kundi la Sungusungu Busule Likimwaga utamu wa burudani.
Shughuli za Uzinduzi zimefanyika sambamba na vikundi mbalimbali vya ulinzi shirikishi yaani Sungusungu kupita mbele ya meza kuu iliyokuwa imesheheni wakuu wa Wilaya zote za mkoa wa Mwanza na Sekta mbalimbali za serikali, vikitoa ujumbe kupitia nyimbo kuapa kushirikiana na serikali katika suala zima la ulinzi.
Kundi la Sungusungu Kimiza.
Mgeni rasmi katika sherehe hizo za uzinduzi alikuwa Mkuu wa wilaya Geita Mh.Filemon Shelutete ambaye katika hotuba yake amewataka watanzania hususani vijana katika kipindi hiki cha kuadhimisha miaka hamsini ya uhuru wa nchi, kufuata misingi aliyotuachia Baba wa taifa Hayati MWALIMU JULIUS NYERERE ikiwemo kudumisha umoja kwani ndio njia pekee ya kuleta maendeleo kwa nchi yetu. Aidha amesema mtaji mkubwa kwa taifa lisilo tajiri kama TANZANIA ni kuhakikisha umoja unalindwa kwa nguvu zote..
Wadau hawa wa ulinzi walijiandaa kweli kweli kutia nakshi sherehe hizo za ufunguzi kwa mikogo, mwendo wa madaha sambamba na nyimbo zao tamu za makabila ya kisukuma.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Ngudu Lugulu.
Ni miaka 50 ya Uhuru inakwenda kutimizwa rasmi tarehe 9desemba2011 na wilaya ya kwimba haina maji, visima vya kupampu maji vilivyojengwa na ESAWA vyote ni vibovu vimeharibika.
Matanki tegemewa ya maji kwa wilaya nzima.
Wilaya nzima inamatanki mawili ya maji yaliyojengwa enzi za Ukoloni kwa hesabu ya kuwakimu watu Elfu tatu miaka hiyo ambapo sasa idadi imeongezeka. Malambo ya maji ambayo wananchi walikuwa wakiyategemea yamekauka mapema tena katika msimu wa mvua, Jeh kiangazi kikianza itakuwaje?
Kwaya ya Mawe Matatu ikitumbuiza katika sherehe hizo za uzinduzi.
Unaona Utaaaaamu!
Kasheshe ilizuka pale moja kati ya nyoka hao alipowekwa juu ya meza ya wagenirasmi, si waheshimiwa wakaingia mitini!!.
Filamu la kusisimua... Akiwa ameakti kama kagongwa na nyoka aka Snake.
Wanafunzi wa shule mbalimbali Wilayani Kwimba wakiimba wimbo wa 'Tanzania nakupenda kwa moyo wote'
Wadau wa Chama cha Mapinduzi ambao walijitokeza viwanjani hapo hapa wakishiriki kuimba wimbo wa Taifa ulioongozwa na alaiki ya wanafunzi wa shule mbalimbali wilayani Kwimba.
Halaiki ya wanafunzi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.