ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, September 22, 2016

BAADA YA MWANZA KILIMANJARO QUEENS WATUA DAR NA MAPOKEZI YA NGUVU.

Kilimanjaro Queens imekanyaga ardhi ya Dar ikiwa na kombe la CECAFA Women’s Championship 2016 walilolitwaa nchini Uganda kwa kuifunga timu ya taifa ya wanawake ya Kenya Harambee Starlets kwa magoli 2-1.
Timu hiyo imepeta mapokezi kutoka kwa viongozi wa serikali kupitia Wizara yenye dhamana ya michezo, viongozi wa TFF pamoja na mashabiki ambao walijitokeza kwenye uwanja wa ndege wa Mw. JK Nyerere.
 Safari ya Kilimanjaro Queens ilianza Septemba 9 ikiongozwa na kocha mkuu wa timu hiyo Sebastian Nkoma walikabidhiwa bendera ya taifa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera tayari kuelekea Jinja nchini Uganda baada ya kuhitimisha kambi ya siku chache mjini Bukoba.
 Kabla ya kuelekea Jinja, Kilimanjaro ilicheza mchezo mmoja wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Burundi na kufanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-0.

Wanadada hao wa Tanzania bara waliwasili Uganda wakiwa tayari kukipiga kwenye michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa wanawake katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati. Tanzania iliangukia kwenye Kundi B kundi lililokuwa na timu tatu (Tanzania, Rwanda na Ethiopia).

Ilianza kwa ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Rwanda kisha ikatoka suluhu na Ethiopia na kufanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali kwa matokeo ya kurushwa shilingi kufuatia kulingana pointi na Ethiopia.
 Kwenye husu fainali wakakutana na wenyeji wa mashindano hayo timu ya Uganga ambapo Kilimanjaro ikafuzu hatua ya fainali kwa kuichapa Uganda kabla ya kuishinda Kenya na kutangazwa mabingwa wa CECAFA ya wanawake.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.