Airtel yawafikia wafanyabiashara zaidi ya 150 Magogoni Feri
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa Airtel FURSA leo imewawezesha wafanya biashara zaidi ya 150 wa maeneno ya magogoni sokoni kuendesha biashara zao chini ya kuvuli baada ya kampuni hiyo kukabidhi miamvuli ya biashara kwa wafanya biashara wadogo wadogo kwa lengo la kuboresha maeneo yao ya biashara.
Wafanyabiashara hawa wa bidhaa mbalimbali ambazo ni pamoja na samaki, mboga za majani , soda, maji, na nyingine nyingi wamekuwa wakipigwa na jua kali na baadhi ya bidhaa zao kuathiriwa na jua kali na mvua. Airtel kupitia Airtel FURSA imeona ni vyema kuwawezesha kwa kuwapatia miavuli ya biashara itakayokinga uharibifu wa bidhaa zao na afya zao kwa ujumla
Vifaa hivyo vimekabithiwa na Airtel na kupokelewa na mbunge wa Ilala, Mh. Musa Zungu kwaniaba ya wakazi na wafanyabiashara wa maeneo hayo
Akiongea wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, mbunge wa Ilala, Mh. Musa Zungu alisema “nafurahi kuona Airtel wamejitoa kuwasaidia wafanyabiashara hawa kuendesha biashara zao, msaada huu unathibitisha dhamira ya Airtel ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo wadogo kuendesha biashara zao ili kukuza kipato na kuinua maisha yao.
Miavuli inayotolewa na Airtel leo itawasaidia wafanyabishara hawa kujikinga na jua kali la Dar es salaam na wakati mwingine mvua”
Nachukua fursa hii kuwapongeza Airtel kwa juhudi zao mbalimbali katika kuwasaidia wafanyabiashara kupitia program yao ya Airtel FURSA. Na nNatoa wito kwa makampuni mengine kuiga mfano huu , haijalishi kiasi gani tunatoa kwani kidogo kile tunachotoa kitasaidia sana kukuza biashara za wajasiriamali hawa wadogo wadogo.”
Kwa upande wake Meneja huduma kwa jamii, Bi Hawa Bayumi alisema “ Airtel ni kampuni inayoamini katika kusaidia jamii katika maeneo tunayoendesha biashara zetu . Kwa kupitia mpango wa Airtel FURSA kwa mara nyingine tunatoa msaada kwa wafanyabiashara wa wadogowadogo Kivukoni kwani tunaamini mtu yeyote anaweza kufanya biashara pale atakapowezeshwa , kupewa motisha, na pindi yeye mwenye atakapokuwa na nia dhabiti, kujituma na malengo sambamba na nidhamu katika kazi”.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.