ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, September 22, 2016

KILL QUEENS WAPOKELEWA MWANZA.

Mwenyekiti wa chama cha Soka wanawake Taifa(TWFA) Amina Karuma mbele ya meza kuu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela (wa pili kutoka kulia) akizungumza jinsi walivyokabiliana na changamoto za uendeshaji timu hatimaye kuutwaa ubingwa.
Wawakilishi wetu.
Wawakilishi wetu.
Wachezaji wa timu ya Kilimajaro Queens wakiwa wanamsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (hayuko pichani)
NA ANNASTAZIA MAGINGA, Mwanza

Mwenyekiti wa chama cha Soka wanawake Taifa(TWFA) Amina Karuma amewaomba wadau kuwekeza kwenye  soka la wanawake ili kuendeleza ushindi kwenye michuano mingine ya kitaifa na kimataifa.

Timu ya Kilimanjaro Queen’s ilitwaa ubingwa wa kombe la chalenji (CECAFA) baada ya kuifunga timu ya harambee starlets ya Kenya mabao 2-1 kwenye mchezo wa fainali wa michuano hiyo kwa nchi za Afrika mashariki.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mara baada ya kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, Mwenyekiti huyo amesema timu ya mpira wa miguu ya wanawake haina utofauti na soka la wanaume hivyo hawana budi kuwekeza kwenye upande huo na kwamba kombe hilo sio la Kilimanjaro Queens bali ni la nchi nzima.

“Makapuni mbalimbali wawekeze kwenye timu za wanawake wanaocheza soka tazama leo Kilimanjaro Queen’s imetutoa kimaso maso na kuipa nchi yetu hadhi ya kimataifa”amesema Amina.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amesema timu hiyo inastahili heshima ya kipekee na kwamba hawajapata kombe la kimataifa hivi karibuni na kuahidi kutoa Sh milioni moja ambayo iliekeezwa kwenye chama cha soka la wanawake Mkoani Mwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.